Na walter mguluchuma
Mpanda
Mtoto mmoja
mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa Kijiji
cha Majalila wilaya ya Mpanda ameuwawa kwa kupigwa na fimbo kwenye sehemu
mbalimbali za mwili wake na baba yake wakambo
aitwaye Hamisi Mohamed.
Tukio hilo
lilitokea hapo juzi majira ya usiku
wakati moto huyo alipokuwa amelala
kitandani na wazazi wake
Kwa mujibu
wa kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari alisema marehemu
huyo alikufa baada ya baba yake wa kambo kukasilishwa na kitendo cha mtoto huyo
kulia wakati akiwa amelala kitendo ambacho aliona kinamnyima usingizi.
Alisema
kitendo hicho cha marehemu kulia
kilimfanya baba huyo wa kambo kimkasilishe na ndipo alipoanza kumpiga fimbo
sehemu mbalimbali za mwili wake huku mama wa motto akimsihi baba huyo wa kambo
aache kumpiga mtoto huyo.
Alieleza
baada ya kuona hari ya motto huyo imekuwa mbaya baba huyo wa kambo alimuaga
mkewe kuwa anakwenda dukani kumnunulia dawa
za maumivu.
Baada ya
baba huyo wa kambo kwenda dukani motto huyo alifarikibaada ya muda mfupi toka
baba yake huyo wa kambo alivyokuwa amekwenda dukani ambapo alitokomea kusiko
julikana.
Kamanda
Kidavashari alisema uchunguzi wa awali
wa baba wa kambo kumuuwa mtoto
huyo ni chuki baina ya mama wa mtoto huyo aitwaye Diana Philipo na mume wake
ambae akutaka marehemu aishi nyumbani kwake.
Jeshi la
polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa aliakikamatwa afikishwe kwenye vyombo
vya sharia

0 comments:
Post a Comment