Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Eng. Emmanuel Kalobelo akifubgua mafunzo
ya siku mbili ya utafiti wa wanafunzi wasio jua kusoma , kuandika na
kuhesa katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mpanda.
Picha na Walter Mguluchuma
Na Walter Mguluchuma
Mpanda -Katavi yetu Blog
Zaidi ya wanafunzi elfu tano wanaosoma katika shule za msingi katika
Mkoa wa Katavi wakiwa wanasoma darasa la pili hawajuwi kusoma
kuandika na kuhesabu
Hayo yalisemwa hapo juzi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi
Emanuel Kalobelo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya
utafiti wa matokeo ya ujifunzaji kwa watoto wa miaka saba hadi
miaka kumi na sita yaliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoriki
jimbo la Mpanda
Mafunzo hayo yaliyo andaliwa na shirika lisilo la Kiserikali
linaloitwa (UWEZO TANZANIA) yanawashirikisha washiriki kutoka
Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wa Katavi ambazo ni Halmashauri
ya Mlele, Nsimbo, Mpanda na Halmashauri ya Mji wa Mpanda
Mwandisi Kalobelo alisema kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya wanafunzi
5,855 ambao hadi sasa wanao soma darasa la pili wakiwa hawajuwi
kusoma kuandika na kuhesabu
Alisema lengo la Mkoa wa Katavi ni kuhakikisha kwamba wanafunzi
wanajua kusoma na kuandika wakiwa Darasa la pili
Pia alisema mkoa umepanga kuinua ufaulu wa mitihani wa kumaliza
elimu ya msingi kufikia asilimia 60% mwaka huu ambapo ufaulu wa
mwaka jana kwa wanafunzi wa darasa la saba ulikuwa ni asilimia 26%
Alifafanua kwa shule za Sekondari wamepanga kuinua ufaulu wa mtihani
wa kidato cha nne kufikia asilimia 60% mwaka 2013 kutoka asilimia 42%
za mwaka 2012 na asilimia 70% mwaka 2014 na asilimia 80% mwaka 2015
Alisema ili kufikia malengo hayo Mkoa umepanga mikakati wa upangaji
wa shule kuwa katika madaraja na kutangaza matokeo ya mitihani ya
kila shule kwenye vyombo vya habari na mbao za matangazo pamoja na
kutowa tuzo kwa shule zinazofanya vizuri
Mikakati mingine ni kutowa motisha kwa walimu ,kuwapa mafunzo ya mara
kwa mara waalimu ,kuwepo kwa ruzuku ya uendeshaji wa shule na
ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule
Kalobelo alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu katika
Mkoa wa Katavi ni utoro wa wanafunzi, uhaba wa miundombinu kama
vile nyumba za walimu, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo
Changamoto nyingine ni upungufu wa walimu hasa wa shule za sekondari
kwani waliopo kwa sasa ni 762 ambao ni sawa na asilimia 68% wakati
mahitaji ya walimu wa shule za sekondari ni 1,121 pia bado kuna tatizo
la uhaba wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia
Kwa upande wa shule za msingi waliopo ni asilimia 96% tatizo lililopo
ni walimu kupangwa bila kuzingatia mahitaji ya waalimu kwani shule
nyingine zimekuwa zikipangiwa waalimu waalimu wengi bila kujali
mahitaji yao hivyo ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi
kupanga waalimu kwa kuzingatia mahitaji
Kwa upande wake Mratibu wa UWEZO wa Mkoa wa Katavi Godfrey Mogellah
alisema mafunzo hayo yamekuwa yakifanyika kwa kipindi cha miaka
minne sasa katika nchi tatu za Tanzania , kenya na Uganda na mwaka
huu mafunzo hayo yanafanyika kwa wilaya 133 hapa nchini
Alisema mara baada ya kupata mafunzo hayo watafanya utafiti kwenye
shule mbalimbali na kwenye mitaa na vitongoji ili kuweza kuwabaini
wanafunzi walioko mashuleni na majumbani ambao hawajuwi kusoma,
kuandika na kuhesabu
0 comments:
Post a Comment