Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Katavi imemfikisha
mahakamani mwenyekiti wa Baraza la Kata ya Kapalala Tarafa ya
Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani hapa Salvatory Mwanakatwe (63) kwa
tuhuma za kuomba Rushwa ya ngono
Kwa mijibu wa mkuu wa Takukuru Mkoa wa
Katavi John Minyenya mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa
hilo mnamo Agosti 11 mwaka juzi katika nyumba ya kulala
wageni inayoitwa Mawenzi iliyoko katika mtaa wa mji mwema
Mtuhumiwa anadaiwa akiwa mwenyekiti wa
Baraza la Kata alitumia wadhifa wake kutenda kosa la kumshawishi na
kumwomba Rushwa ya ngono mwanamke mmoja ambae jina
limehifadhiwa ili amsaidie katika shauri lake dhidi ya mumewe ambae
alikuwa amemshitaki kwenye Baraza hilo kwa kumtelekeza na kisha kuuza
mali walizochuma pamoja
Minyenya alieleza mbele ya waandishi wa
habari kuwa mwanamke huyo baada ya kuombwa Rushwa hiyo ya ngono
akuridhika na kitendo hicho cha kutoa rushwa ya ngono kwa mwenyekiti wa
Baraza la Kata
Alisema ndipo alipofikisha taarifa kwenye
Taasisi ya kupambana na Rushwa Mkoani Katavi kuhusiana na
tuhuma za Salvatory Mwanakatwe kudai apewe Rushwa ya ngono na
mwanamke huyo
TAKUKURU baada ya kupokea taarifa hizo ilianza
kufanya uchunguzi juu ya rushwa hiyo ya ngono na iliweza kubaini
kuwa tuhuma hizo zilizotolewa na mwanamke huyo ni za kweli
Alisema
ndipo Maafisa wa TAKUKURU walipoandaa mtego wa Rushwa dhidi ya
mshitakiwa Salvatory hapo mnamo Agosti 11 2011 na kufanikiwa
kumkamata mtuhumiwa akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Mawenzi
Katika mtaa wa Mji Mwema akiwa na mwanamke huyo
Mshitakiwa amefikishwa mahakamani na
kusomewa shitaka la kuomba rushwa ya ngono ikiwa ni kinyume na
kifungu cha sheria cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na
Rushwa namba 11ya mwaka 2007
Mshitakiwa baada ya kusomewa
mashitaka yanayomkabili dhidi yake alikana kutenda kosa hilo hata
hivyo mtuhumiwa alikwenda rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti
ya dhamana
Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi alieleza kuwa kesi
hiyo imechelewa kufunguliwa kutokana na taratibu zilizopo sasa
ambapo kesi zote zinazofunguliwa na Takukuru mahakamani lazima kibali
kitoke kwa mwanasheria mkuu wa Serikali
Aidha TAKUKURU imetowa wito kwa
wananchi wote kuzingatia maadili na kutojihusisha na vitendo
vya Rushwa wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku
wakati wanapodai haki zao kwani Rushwa ni adui wa
haki hivyo Rushwa haikubaliki
0 comments:
Post a Comment