Baadhi ya watumishi wa Idara ya Afya katika hospitali ya wilaya ya
Mpanda Mkoa wa Katavi wametishia kujiondoa katika mfuko wa shirika la
jamii la NSSF kwa kile wanacho dai mfuko huo hauna manufaa kwa
watumishi
Kauli hii ilitolewa hapo jana
na watumishi hao wa Idara ya afya kwenye mkutano
ulio fanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya wilaya ya Mpanda
ulio hudhuriwa pia nameja wa Nssf wa Mkoaa wa Katavi na Rukwa pamoja na
viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa mkoa huu
Hatua hiyo ya wafanyakazi
kutishia kugoma imekuja baada ya baadhi ya wafanyakazi wa
idara hiyo ambao walisitaafu hapo mwaka jana kulalamikia malipo
madogo waliyo lipwa na mfuko huo wa jamii
watumishi hao
walidai kuwa watumishi wenzao waliositaafu mwaka jana ambao
walifanya kazi kwa muda wa miaka kati ya 30 na 33 baadhi yao wamelipwa mafao ya
kusitaafu shilingi laki nane na wengine
wamelipwa shilingi milioni mbili wakati wenza waliokuwa wanapata
mshara sawa na wao waliostaafu mwaka jana wamelipwa na mfuko wa LLPF kiasi cha
shilingi milioni 28
Mmoja wa wa watumishi hao
Joice Ngonyani alieleza kuwa wamekatishwa tamaa na malipo kidogo
walio lipwa wenzao mwaka jana hivyo ni vizuri kuanzia sasa
watumishi wa idara hiyo wakajiondoa kwenye mfuko huo wa ajami kauli hiyo
ambayo pia iliungwa mkono na watumishi hao wa afya
Alifafanua kuwa
inasikikitisha mno kwa mtumishi aliye fanya kazi kwa
kipindi cha miaka 33 kama ambavyo alifanya kazi mtumishi mwenzao ambae
alisitafu mwaka jana aitwaye Antonia Kapokele amabaye alilipwa
mafao yake na mfuko huo kiasi cha shilingi milioni mbili tuu wakati
walikuwa wanachangia kwenye mifuko mingine walilipwa kiasi kikubwa
cha pesa
Kwa upande wake mwenyekiti wa Tughe
wa Mkoa wa Katavi Gasto Sesa alisema kuwa kutokana na watumishi hao
wasitaafu kulipwa mafao kidogo walikuwa wameamua kuwaondoa
wanachama wao kuchangia kwenye mfuko huo
Nae meneja wa Nssf wa mikoa ya Katavi
na Rukwa Wiliamu Tutambi aliwaeleza watumishi hao kuwa
tatizo la wasitaafu hao kulipwa mafao kidogo linaweza lika ilmesababishwa
na waajiri wao kutowasilisha mafao yao kwenye mfuko wa jamii
Alisema kuwa ni
kosa la jinai kumshawishi mtu kujiunga na mfuko mwingine wa
shirika la jamii hivyo anae kiuka hupata adhabu ya kulipa faini ya
shilingi milioni kumi au kifungo cha miaka 3 jela hivyo
watumishi hao hawana haki tena ya kujitowa kwenye mfuko wa Nssf
Hata hivyo kauli hiyo ilipingwa
vikali na watumishi hao amba walidai kuwa wanahaki kujiunga na mfuko mwingine
pale wanapo ona mfuko wanao changia hauna manufaa kwao pia walieleza
kujumu la kufatilia michango kwa mwajiri ambae hawasirishi michango
sio la mtumishi bali ni mfuko wenyewe wa shirika la jamii
0 comments:
Post a Comment