Home » » WIMBI LA MATUKIO YA HATARI YAZIDI KUIKUMBA KATAVI: MWILI WA MAREHEMU WAKUTWA UKIWA UMENYOFOLEWA MAZIWA, JICHO NA MDOMO‏

WIMBI LA MATUKIO YA HATARI YAZIDI KUIKUMBA KATAVI: MWILI WA MAREHEMU WAKUTWA UKIWA UMENYOFOLEWA MAZIWA, JICHO NA MDOMO‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Jeshi la polisi mkoa wa katavi linawasaka watu walio nyofoa viungo vya mwili wa marehemu Athama Athumani(40) mkazi wa kijiji cha kabungu aliefariki nyumbani kwake Februari 9  mwaka huu.

Kaimu kamanda wa Geshi  la Polisi Mkoa wa Katavi Joseph Myavela alisema  Marehemu huyo arifariki nyumbani kwake siku  hiyo majira ya saa 12:30 Asubuhi.

Mgovela Mijema ndugu wa Marehemu walifika nyumbani kwa Marehemu ambaye alikuwa akiishi peke yake kwa lengo la kumujulia hari majira hayo ya Asubuhi.

Alifafanua kuwa Baada ya ndugu hao kufika nyumbani kwa marehemu walimukuta akiwa Amefariki Dunia  huku akiwa amelala kitandani kwake.

Alisema baada  ya kumuchunguza mwili wa marehemu warikuta mwili wake  ukiwa umenyoforewa badhi  ya viungo vya mwili wake.

Kaimu Kamanda Myovela alivitaja viungo vya mwili wa marehemu huyo vilivyo kuwa vimenyofolewa kuwa ni chuchu ya Titi la kulia sehemu ya chini yam domo wake jicho moja la upande wa kulia na kukwanguliwa kwa chini ya miguu.

Alisema  uchunguzi wa awali umebaini kuwa Marehemu muda  mfupi baada ya kufariki mtu,watu walifika na kumukata viungo hivyo katika mwili wake.

Kaimu kamanda aliseza kuwa inasadikika chanzo cha kuchukuwa viungo ivyo vya marehemu inatoka na imani  za kishirikina.

Jeshi laPolisi  mkoa wa Katavi kwa kushirikia na Raiya wema linaendelea na msako wa kuwabaini walio fanya vitendo hivyo vya kinyama.

Myovela alieleza mwili wa Marehemu huyo alizikwa siku hiliyofuata katika Makabuli ya kijiji cha Kabungu baada ya mwili wa Marehemu kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa