Home » » AFARIKI DUNIA WAKATI WAKIFANYA IBADA YA MATANGA YA MUMEWE‏

AFARIKI DUNIA WAKATI WAKIFANYA IBADA YA MATANGA YA MUMEWE‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda – Katavi
Mwanamke mmoja Makulata Nsawiyo (68) mkazi wa mtaa wa Kashaulili wilayani mpanda mkoani katavi amefariki dunia wakati wa ibada ya kumalizia matanga ya mumewe Gregoli Kinyonto.

Tukio hili limetokea hapo jana nyumbani kwa marehemu huyo majira ya saa 5:20 asubuhi na kuwafanya waombiolezaji wa msiba huo washindwe kuamini kilichotokea.
Mume wa mama huyo alifarika hapo January 24 mwaka huu na kuzikwa juzi katika makaburi  ya mwangaza yaliyopo mtaa wa makanyagio.
Baada ya mazishi kumalizika hapo juzi wanandugu walipanga kumaliza msiba huo hapo jana majira ya saa 5:00 asubuhi.
Majirani na marafiki wa familia hiyo walifika kama kawaida msibani hapo kwa lengo la kumaliza matanga ya msiba wa Gregoli.
Kama ambavyo ilivyokuwa imepangwa waombolezaji walianza kwa ibada ya kumwombea marehemu iliyokuwa ikiongozwa na mwali wa dini wa Kigango hicho cha Kashaulili.
Wakati ibada inakaribia kumalizika ghafla mama huyo alianguka na kuwafanya waombolezaji washikwe na mshituko hari ambayo ilisababisha ibaada ishindwe kuendelea.
Waombolezaji na wanandugu waiamua kumchukua mama huyo na kumkimbiza katika hospitali ya wilaya yam panda kwa ajiri ya matibabu.
Hata hivyo wakati wakiwa bado wako njiani mama huyo arifariki dunia na  kabla ya kufikishwa katika hospitali na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa