Home » » WAKAZI WA KIGAMBONI WAWEKEWE KIVUKO

WAKAZI WA KIGAMBONI WAWEKEWE KIVUKO


 Na Walter Mguluchuma
        Mpanda - Katavi. 

WAKAZI wa eneo la  Kigamboni  lililopo  katika kata ya Makanyangio  katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi  wameiomba serikali iweze kuwajengea kivuto kutokana na kivuko kilichopo   kotohimili mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini na hivyo kuwaweka katika  hatari ya kusomwa na maji.


Wakizungumza na Gazeti hili  wakazi hao wamesema kuwa kutokuwa  na kivuko imara katika eneo hilo la kawajense kumekuwa kukihatarisha maisha yao na maisha ya wagonjwa huku wanafunzi wengi wakishindwa kuhudhuria masomo yao kutokana na kushindwa kuvuka katika eneo hilo lililojengwa daraja la chini na hivyo kuishauri serikali kujenga daraja la juu.

Wakazi hao wamesema kuwa hivi sasa katika kipindi cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini kumesababisha daraja hilo kutopitika na hivyo kuwapa wakati mgumu wa kuendesha shughuri zao za kuwaendeshea kipato huku wakiofia pia masiaha yao kutoka na daraja hilo kujaa maji kila wakati.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Makanyagio Bw Iddy Nziguye amesema kuwa mpaka sasa wamekwisha fanya mawasiliano na idara ya ujenzi katika halmashuari ya mji wa mpanda kwa lengo la kunusuru maisha ya wakazi hao ,huku mkurugenzi wa halamshauri hiyo Bw Joseph Mchina akisema kuwa barabara  hiyo ipo katika mpango wa ujenzi katika mwaka huu wa fedha,ikiwa ni pamoja na ofisi za wabunge wa jimbo la mpanda mjini.

Bw Mchina amesema kuwa mpaka sasa zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo ya kigamboni  hadi makanyagio imekwishatangazwa na wakati wowote kaunzia sasa ujenzi wa barabara hiyo pamoja na daraja vitajengwa. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa