ZIKIWA zimepita takribani siku tatu baada cha chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mikoa ya Rukwa na Katavi kutoa tamko kwa vyombo vya habari la kumvua madaraka Mwenyekiti wa baraza la Vijana wa mikoa hiyo Bw Laurent Mangweshi huku akiwa hajakabidhiwa barua ya kimaandishi inayohusu kuvuliwa madaraka amesem kuwa mara baada ya kukabidhiwa barua yake atakata rufaa kwa lengo la kupata haki yake.
Akizungumza na gazeti hili kwa ya Simu Magweshi’amesema kuwa mpaka sasa swala la kuvuliwa kwangu madaraka nalisikia tu katika vyombo vya habari na wadau wangu wengine lakini nakiri kuwa mpaksa sasa sina barua wala kieelezo chochote kinachoonyesha kuwa nimevuliwa madaraka ndani ya chama na hivyo nasema kuwa taaarifa hizo zilizozagaa mitaani ni uzushi tu mie bado ni mwenyekiti wa baraza za vijana wa mikoa ya Rukwa na Katavi alisema Magweshi
.
Alopohojiwa juu ya kuonywa mara kadhaa katika vikao kutokana na utovu wa nidhamu alisema kuwa katika maisha yake hajawahi kuonywa na tangu kujiunga kwake ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo mwaka 2001 hakuna kikao cha Baraza la Uongozi lililokaa na kufafanua kuwa baraza la Usuruhisho hallina mamlaka ya kutoa adhabu wala kumvua mtu madaraka na kusema kuwa kikao cha mjini Namanyere kilikuwa ni cha baraza la Usuruhishi na si cha barala la uongozi lenye mamlaka.
Hata hivyo Bw Magweshi alihoji kwanini viongozi hao wamekimbilia katika vyombo vya habari na kutoa Tamko kabla ya kukamilisha taratibu zote za kichama ikiwemo ile ya kuandikiwa barua na kuongeza kuwa yeye ndiye aliyepaswa kukimbilia katika vyombo vya habari kwa lengo la kutafuta haki yake endapo angekabidhiwa barua na si viongozi hao.
Alipohojiwa juu ya hatua gani atazichukua endapo ataona haki yake haijatendeka ndani ya chama hicho je atakuwa na mpango wa kuondoka ndani ya chama hicho na mwelekeo wake ni chama kipi? Mangweshi alisema kuwa sina mpango wowote wa kuhihama chadema mimi nitafia chadema kwa kuwa chadema nia yake ni kulikomboa taifa toka katika chama cha mapinduzi na kuleta mabadiliko ya kweli na mimi nakuhakikishia kuwa ni Chadema Original naipenda sana chadema ila siwezi kukubali kukiaibisha chama changu na wala sina njaa za kuhamahama vyama alisema Magweshi.
Alisema kuwa’nawaheshimu sana viongozi wangu na nitaendelea kufanya kazi kwa lengo la kukijenga chama na nasema kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu kwa asilimia mia moja bali kila binadamu namapungufu yake.
Hata hivyo kufuatia taarifa hiyo ya kutokabidhiwa kwa barua kwa wakati mwenyekiti huyo wa baraza la vijana anayedaiwa kuvuliwa madaraka kutokana na sababu mbalimbali gazeti hii lilifanikiwa kufanya mahojiano na Katibu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Mikoa ya Rukwa na Katavi Bw Ozem Chapita ambaye licha kukiri kucheleweshwa kwa tukio hilo la kumkabidhi barua alifafanua kuwa hali hiyo imetokana na mazingira ya kazi kutoakana hali ya mwenyekiti huyo kuishi mkoani katavi huko katibu huyo ambaye ni mtendaji mkuu akiwa anaishi mkoani Rukwa.
Hata Hivyo Chapita alisema kuwa mpaka sasa amekwisha fanya utaratibu wa kusafirisha barua hiyo kwa njia ya Basi ili iweze kumfikia Magweshi.
0 comments:
Post a Comment