Home » » JUMLA YA WATU NANE WAMEFARIKI DUNIA KATIKA KIPINDI CHA MIEZI SITA KTUKANA NA AJALI 145 ZA BODABODA NA WATU 82 WALIJERUHIWA

JUMLA YA WATU NANE WAMEFARIKI DUNIA KATIKA KIPINDI CHA MIEZI SITA KTUKANA NA AJALI 145 ZA BODABODA NA WATU 82 WALIJERUHIWA


Na Walter Mguluchuma
Mpanda.
Jumla ya watu nane wamefariki dunia katika ajari 145 zilizotokea mkoani Katavi kutokana na ajari za bodaboda na kusababisha watu 82 kuwa majeruhi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashar alisema matukio hayo yote yametokana na uzembe wa waendesha pikipiki (bodaboda).
Alisema mwezi june zilitokea ajari 17 na majeruhi 11, mwezi Julai ajali 21 majeruhi saba ambapo mwezi Agosti ajari zilikuwa 37 majeruhi 15 na vifo vya watu 3.
Alieleza mwezi Septemba zilitokea ajari  zina watu 21 wakapata majeruhi na kifo cha mtu mmoja Mwezzi Oktoba ajali zilikuwa 14 na majeruhi 14 na kifo cha mtu mmoja na mwezi Novemba kulitokea ajari 29 na majeruhi 15 na watu watatu walikufa.
Kamanda Kidavashari alisema katika kukabiliwa na tatizo la kuongezeka kwa ajali za bodaboda jeshi la polisi  mkoa wa kataviumeisha anza mikakati ya kupunguza ajari hizo
Aliitaja mikakati hiyo ni kutowa mafunzo kwa bodaboda wote kupitia vyuo vya veta.
Ambapo tayari ameisha anza kutoa mafunzo kwa bodaboda ili kila mmoja awe na leseni ya udreva.
Pia wamefanya  usajiri wa kila bodaboda na kila kituo kina kiongozi wao wa eneo la kituo
Alitaja mkakati mwingine ni wa kutoa namba kwa kila kituo cha bodaboda katika mkoa wa Katavi kimepewa namba ya usajiri na inapokuwa imetokea ajari imekuwa ikiwapaaskali wa usalama barabarani kujua bodaboda ni kituo gani.
Pia alieleza jeshi hilo limepunguza kutoa adhabu ya faini ba badala yake bodaboda ambaye amepatikana na makosa sasa hivi wamekuwa wakifikishwa mahakamani na kupewa adhabu ya kifungo cha kuanzia miezi 3 hadi mwaka mmoja
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limetoa kwa bodaboda wote kwa mafunzo ya VETA ambapo wamepunguziwa gharama kutoka sh. 60,000 za gharama za mafunzo hadi kufikia sh. 20,000 na mafunzo hayo yanayotolewa na VETA yamekuwa yakifanyika katika vituo wanakofanyia shughuli zao.
Amevitaja vituo hivyo kuwa ni Kituo cha Majimoto kilichoopo tarafa ya Mpimbwewilayani Mlele na vituo vya Mpanda Mjini kwenye maeneo wanayofanyia shghuli mabodaboda.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa