Home » » AUWAWA WAKATI AKIAMUA UGOMVI WA WANYWAJI WA POMBE YA KIENYEJI NYUMBANI KWAKE

AUWAWA WAKATI AKIAMUA UGOMVI WA WANYWAJI WA POMBE YA KIENYEJI NYUMBANI KWAKE


Na walter mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja  mkazi wa kijiji  cha  Itetemiya  Tarafa ya Karema wilayani Mpanda  mkoa wa Katavi  Joseph  Kiloloma (45)  ameuwawa kwa kupigwa na fimbo  kichwani  wakati  akiamua ugovi  wa watu wawili  walio  kuwa   wakinywa pombe ya kienyeji  nyumbani kwake
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi  Dhahiri  Kidavashari   alisema  mtu  huyo  aliuwawa hapo juzi  majira ya saa  3 usiku  nyumbani  kwa marehemu huyo
Alisema katika tukio hilo   marehemu  huyo  akiwa  nyumbani  kwake   akiwa anafanya  biashara  ya kuuza pombe  ya kienyeji  aina  ya komoni  kisha walitokea  wateja hao wawili walio fika hapo   ili waeweze kupatata huduma hiyo  ya pombe  ya kienyeji
Joseph  alianza kuwapa huduma huduma hiyo  ya pombe  wateja wake  hao   na huku   wa wakiwa   wanakunywa  na wakati huo wakiendelea  na mazungumzo  yao
 Kidavashari alieleza kuwa  ghafla wateja  hao  walianza mabishano  ambayo  yalipelekea  watu hao  waanze  ugomvi  wa kupigana
 Hari  ambayo  ilimfanya  Joseph  ambaye  alikuwa mwenyeji  wao  aingilie  kati ugomvi  huo   kwa  kuwaomba waache  kupigana  na kisha  aliwaamu   na wakaacha  ugomvi
Kidavashari   alieleza watu  hao  baada ya kuamuliwa  ugomvi   walimgeukia  Joseph  na walianza kumpiga  kwa fimbo  kichwani  na kumfanya apige mayowe ya kuomba msaada kwa majirani
 Hata hivyo watu  hao  waliendelea  kumshambulia   na kisha walipo   ona  majirani  wanakuja  waliamua kutimua  mbio  kuelekea  vichakani
Alieleza kuwa majirani hao waliamua kumkimbiza   Joseph  katika   hospital ya tarafa ya Karema  wakati    wakiwa njiani  arifariki dunia
 Kamanda  alisema kuwa jeshi la polisi mkoa wa Katavi  linaendelea kuwasaka watu  hao  ambao  majina yao hayakuweza  kufahamika  ili waewze kufikishwa kwenye vyombo vya dora
Alifafanua  kuwa  taarifa za awali   walizo  zipata   zinaonyesha watu walio husika katika tukio hilo wanafamika kwa wakazi wa kijiji  hapo 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa