Home » » WATU 12 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUTEKA BASI LA SUMRY‏

WATU 12 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUTEKA BASI LA SUMRY‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda  Katavi
Watu 12 wanashikiliwa  na jeshi la polisi wilaya ya mpanda  mkoa wa Katavi kwa tuhuma za  kuteka  basi la  la kampuni ya  mabasi ya Sumry mwishoni mwa wiki iliyopita.
Watuhumiwa  hao wanadaiwa  kuteka  basi lenye namba za usajiri  T 902 AZT Nissan Diesel lilikuwa likiendeshwa na  na Khalid Makamba   mali ya kampuni ya mabasi ya Sumry hapo  Oktoba 17 mwaka huu majira ya saa 6 na dakika 23 usiku  katika eneo la Magamba   tarafa ya Nsimbo wilaya ya Mlele.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Joseph Myovela  alisema  siku hiyo  ya tukio hili watuhumiwa hao wa ujambazi  wakiwa na marungu mapanga na nondo  waliweka mawe   barabarani   na  kufanikiwa kuteka basi  hilo  ambalo lilikuwa na abiria  wakitokea Sumbawanga  kuulekea wilayani Mpanda.
Katika tukio hilo  la ujambazi walifanikiwa  kuwapola  abiria hao  simu  pesa  na vitu mbalimbali   ambavyo thamani yake  bado  haijajulikana. 
Myovela aliwataja watuhumiwa hao wanao shikiliwa na polisi kuwa ni   Elias Zakaria  (45) mkazi wa makazi ya wakimbizi ya Katumba,   Mbuya Michael (25), Moses  Liberatus (24) mkazi wa mtaa wa Kawajense, wote wa mjini mpanda,   Jackson Lucas   (27) mkazi wa kijiji cha Katisunga wilayani Mlele, Mussa Nassor (17),  Ramadhani Hassan (17) wakazi wa mtaa wa Majengo wilayani mpanda.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi amewataja watuhumiwa wengine  ni  Abdallah Hassani  (19) mkazi wa mtaa wa Majengo, Joseph Masesa  (22),  Sayo  Masunga  (18),   Christopher  Kwebe  (20),  Elias George (24) wakazi wa majengo mpanda  na  Shaban Loxagune (22) mkazi wa makazi ya wakimbizi ya katumba  wilaya ya Mlele.
Watuhumiwa hao wanadaiwa baada ya kutenda  tukio hilo  la ujambazi  walitokomea kusiko julikana huku wakiwa na mali walizo zipola kwa abiria hao.
Myovela alisema  baada ya  tukio hilo  jeshi la polisi mkoa wa Katavi   liliendesha msako mkali  kwa kushirikiana na wananchi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa   12  wanaodaiwa kuhusika  katika  tukio hilo  la ujambazi.
Watuhumiwa hao bado wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka.
Myovela pia alieleza kuwa  siku hiyo  pia katika eneo hilo  kabla hawaja liteka basi hilo la kampuni ya Sumry waliteka lori  lenye namba za usajiri   T 107 BHT aina ya fuso lilikuwa likiendeshwa na  Said Side  lililokuwa likkitokea tarafa ya Mpimbwe na  kupola simu na vitu mbalimbali.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa