Home » » UZALISHAJI WA ZAO LA TUMBAKU MKOA WA KATAVI WASHUKA KUTOKA KILO MILIONI 15 HADI KILO MILIONI 6‏

UZALISHAJI WA ZAO LA TUMBAKU MKOA WA KATAVI WASHUKA KUTOKA KILO MILIONI 15 HADI KILO MILIONI 6‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda-Katavi
Uzalishaji wa zao la tumbuka   katika mkoa wa Katavi  umeshuka kutoka kilo  Milioni  15,595,493 za  msimu wa kilimo  ulio pita   hadi kufikia kilo Milioni      6,813,025  katika msimu wa kilimo wa mwaka huu.
Hayo yamesemwa hapo jana   na Mteuzi  Mfawidhi wa Bodi ya tumbaku mkoa wa Katavi  Yusuh Mahundi   ofisini kwake wakati akitowa taarifa mbele ya waandishi wa habari  ya ununuzi wa zao hilo.
Mahundi alieleza kuwa  msimu wa mwaka huu wa ununuzi wa zao la tumbaku  ulianza  tarehe  15 Mei  mwaka huu  na kumalizika  tarehe 8 Septemba  ambapo jumla ya kilo  milioni  6,813,025 zilinunuliwa  zikiwa na thamani ya shilingi  Bilioni 12,398,013  ambapo kilo moja ilinunuliwa kwa wastani wa dola 1.82.
Msimiu ulio pita wa kilimo mkoa wa Katavi  ulizalisha jumla ya kilo   milioni 15,595 ,493 za zao hilo yenye thamani ya  shilingi  bilioni  23,051,650  na kilo moja ilinunuliwa kwa wastani wa dola  1.48.
Alisema  msimu huu  uzalishaji  umeshuka kwa kilo  milioni  8,782,467 zenye thamani ya shilingi  bilioni  10,653,636.
Tumbaku hiyo ilizalishwa kupitia vyama vya  ushirika vya msingi  ambavyo alivitaja vyama hivyo kuwa ni  Ilende, Ukonongo, Nsimbo, Katumba, Mpandakati,   Mishamo Tamcos,  na Kampuni ya wakulima wa Mishamo.
Alizitaja changamoto  zilizopo kuwa ni   kuwepo  kwa kiwango  kikubwa cha tumbaku  zenye kasoro ambazo hazina  maslahi  kwa wakulima  na wakulima wengi kulima bila kusajiriwa  na Bodi ya tumbaku.  
Pia wakulima kutorosha tumbaku na kuuzia kwenye vyama vingine vilivyopo jirani  hivyo  kutorosha madeni  yao kwenye vyama  hari ambayo inaua  uhai wa  vyama  na mapato ya wakulima.
Changamoto nyingine  nyingine  alizitaja kuwa ni  wakulima kufunga tumbaku   bila kuwa na usimamizi kwanye vituo vya kufungia na kusababisha   kuchanganywa kwa tumbaku mbaya na nzuri .
Mahundi alieleza kuwa kutokana na changamoto hizo   Bobi ya tumbaku ambao ndio wasimamizi  wakuu wa zao la tumbaku wamejipanga na watahakikisha  vyama vya msingi  vinaandaa masoko kwa wakati.
vilevile  watahakikisha  hakuna soko  litakalo  fanyika msimu ujao  kama tumbaku  haikufungwa kwenye  vituo   vitakavyo kuwa   vimeandaliwa na kusajiliwa na Bodi ya tumbaku.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa