Na Walter Mguluchuma
Mpanda-Katavi
Uzalishaji wa zao la tumbuka katika mkoa wa Katavi umeshuka kutoka kilo Milioni 15,595,493 za msimu wa kilimo ulio pita hadi kufikia kilo Milioni 6,813,025 katika msimu wa kilimo wa mwaka huu.
Hayo yamesemwa hapo jana na Mteuzi Mfawidhi wa Bodi ya tumbaku mkoa wa Katavi Yusuh Mahundi ofisini kwake wakati akitowa taarifa mbele ya waandishi wa habari ya ununuzi wa zao hilo.
Mahundi alieleza kuwa msimu wa mwaka huu wa ununuzi wa zao la tumbaku ulianza tarehe 15 Mei mwaka huu na kumalizika tarehe 8 Septemba ambapo jumla ya kilo milioni 6,813,025 zilinunuliwa zikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 12,398,013 ambapo kilo moja ilinunuliwa kwa wastani wa dola 1.82.
Msimiu ulio pita wa kilimo mkoa wa Katavi ulizalisha jumla ya kilo milioni 15,595 ,493 za zao hilo yenye thamani ya shilingi bilioni 23,051,650 na kilo moja ilinunuliwa kwa wastani wa dola 1.48.
Alisema msimu huu uzalishaji umeshuka kwa kilo milioni 8,782,467 zenye thamani ya shilingi bilioni 10,653,636.
Tumbaku hiyo ilizalishwa kupitia vyama vya ushirika vya msingi ambavyo alivitaja vyama hivyo kuwa ni Ilende, Ukonongo, Nsimbo, Katumba, Mpandakati, Mishamo Tamcos, na Kampuni ya wakulima wa Mishamo.
Alizitaja changamoto zilizopo kuwa ni kuwepo kwa kiwango kikubwa cha tumbaku zenye kasoro ambazo hazina maslahi kwa wakulima na wakulima wengi kulima bila kusajiriwa na Bodi ya tumbaku.
Pia wakulima kutorosha tumbaku na kuuzia kwenye vyama vingine vilivyopo jirani hivyo kutorosha madeni yao kwenye vyama hari ambayo inaua uhai wa vyama na mapato ya wakulima.
Changamoto nyingine nyingine alizitaja kuwa ni wakulima kufunga tumbaku bila kuwa na usimamizi kwanye vituo vya kufungia na kusababisha kuchanganywa kwa tumbaku mbaya na nzuri .
Mahundi alieleza kuwa kutokana na changamoto hizo Bobi ya tumbaku ambao ndio wasimamizi wakuu wa zao la tumbaku wamejipanga na watahakikisha vyama vya msingi vinaandaa masoko kwa wakati.
vilevile watahakikisha hakuna soko litakalo fanyika msimu ujao kama tumbaku haikufungwa kwenye vituo vitakavyo kuwa vimeandaliwa na kusajiliwa na Bodi ya tumbaku.
No comments:
Post a Comment