Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya mpanda mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuteka basi la la kampuni ya mabasi ya Sumry mwishoni mwa wiki iliyopita.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuteka basi lenye namba za usajiri T 902 AZT Nissan Diesel lilikuwa likiendeshwa na na Khalid Makamba mali ya kampuni ya mabasi ya Sumry hapo Oktoba 17 mwaka huu majira ya saa 6 na dakika 23 usiku katika eneo la Magamba tarafa ya Nsimbo wilaya ya Mlele.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Joseph Myovela alisema siku hiyo ya tukio hili watuhumiwa hao wa ujambazi wakiwa na marungu mapanga na nondo waliweka mawe barabarani na kufanikiwa kuteka basi hilo ambalo lilikuwa na abiria wakitokea Sumbawanga kuulekea wilayani Mpanda.
Katika tukio hilo la ujambazi walifanikiwa kuwapola abiria hao simu pesa na vitu mbalimbali ambavyo thamani yake bado haijajulikana.
Myovela aliwataja watuhumiwa hao wanao shikiliwa na polisi kuwa ni Elias Zakaria (45) mkazi wa makazi ya wakimbizi ya Katumba, Mbuya Michael (25), Moses Liberatus (24) mkazi wa mtaa wa Kawajense, wote wa mjini mpanda, Jackson Lucas (27) mkazi wa kijiji cha Katisunga wilayani Mlele, Mussa Nassor (17), Ramadhani Hassan (17) wakazi wa mtaa wa Majengo wilayani mpanda.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi amewataja watuhumiwa wengine ni Abdallah Hassani (19) mkazi wa mtaa wa Majengo, Joseph Masesa (22), Sayo Masunga (18), Christopher Kwebe (20), Elias George (24) wakazi wa majengo mpanda na Shaban Loxagune (22) mkazi wa makazi ya wakimbizi ya katumba wilaya ya Mlele.
Watuhumiwa hao wanadaiwa baada ya kutenda tukio hilo la ujambazi walitokomea kusiko julikana huku wakiwa na mali walizo zipola kwa abiria hao.
Myovela alisema baada ya tukio hilo jeshi la polisi mkoa wa Katavi liliendesha msako mkali kwa kushirikiana na wananchi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 12 wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo la ujambazi.
Watuhumiwa hao bado wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka.
Myovela pia alieleza kuwa siku hiyo pia katika eneo hilo kabla hawaja liteka basi hilo la kampuni ya Sumry waliteka lori lenye namba za usajiri T 107 BHT aina ya fuso lilikuwa likiendeshwa na Said Side lililokuwa likkitokea tarafa ya Mpimbwe na kupola simu na vitu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment