Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Watu wawili mtu na mke wake wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Katavi kwa tuhuma za kukamatwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa katavi Joseph Myovela amewataja watuhumiwa walio kamatwa kuwa ni Justin Jailos (33) mkazi wa mtaa wa Kawajense wilayani mpanda na mwananke mmoja aitwaye Magdalena Kimali (28) mkazi wa mkoa wa Kigoma.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 15 mwaka huu majira ya saa 9 usiku nyumbani kwa Justin katika mtaa wa Kawajense mjini Mpanda.
Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia kupatikana kwa taarifa za siri za kuwepo kwa meno ya tembo nyumbani kwa watuhumiwa walio kuwa wakiishi pamoja.
Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo askari wa hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa kushirikiana na askari polisi walifika nyumbani kwa mtuhumiwa ilikufanya upekuzi kwa kuwashirikisha viongozi wa mtaa husika.
Myovela alieleza baada ya askari kujitambulisha kwa mtuhumiwa na kumweleza nia yao ya kufika kwenye eneo hilo watuhumiwa walikiri kuwepo kwa nyara hizo ndani ya nyumba yao.
Ndipo wao wenyewe walipo ingia ndani ya nyumba nyumba na kutowa nyara hizo za serikali kabla ya kufanyiwa upekuzi zikiwa zimehifadhiwa ndani ya ndoo.
Baada ya kufungua ndoo hiyo ya plastic walikuta vipande vitano vya meno ya tembo ambavyo ni sawa na tembo mmoja mwenye thamani ya shilingi Milioni 22,500,000.
Kaimu kamanda Myovela alisema watuhumiwa wote wawili tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya wilaya ya Mpanda kujibu mashitaka ya kukamatwa na nyara za serikari kinyume cha sheria
0 comments:
Post a Comment