Home » » ‘MAONI YA KATIBA YALENGE KULIJENGA TAIFA’

‘MAONI YA KATIBA YALENGE KULIJENGA TAIFA’

Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima  amewataka  wananchi wa wilaya  hiyo  kutoa maoni ya kuwaunganisha wananchi na sio ya kuwagawa wanapotoa maoni  kwenye mikutano ya tume yakupokea maoni ya marekebisho  ya katiba 
Kauli hiyo aliitowa hapo jana mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kupokea maoni ya marekebisho  ya katibu uliofanyika  katika uwanja wa wa shule ya msingi  nyerere  katika uwanja wa kawajense  alipo zungumza  na mwandishi   wa   habari alisema wapo watu wanao fika kwenye mikutano ya
Tume hiyo ya Taifa inayoongozwa na Dr. ADILIANO MVUNGI wakiwa wakitoa maoni yao kwa kusoma kwenye karatasi.

Alieleza upo uwezekano mkubwa wa watu wasio itakia mema nchi yetu kwa kuwandikia maneno ambayo yanaweza kutugawa.

Mwamlima alisema ni vizuri kila mtu akawasilisha mawazo yake mwenyewe na sio mawazo ya kuandikiwa na mtu mwingine  miongoni mwa mapendekezo yaliyo tolewa na wananchi mbele ya Tume ya Taifa ya kupokea maoni ya marekebisho ya Katiba ni pendekezo la kupunguza muda wa kustaafu kwa watumishi wa Umma kutoka miaka 60 hadi 40.

Pia waliomba watumishi ambao wanakuwa wamemaliza muda wao wasipewe tena nafasi ya kuteuliwa kuwa wajumbe au wenye viti wa Bodi mbalimbali.

Pendekezo jingine waliomba ardhi iwe chini ya wananchi wanao ishi kwenye eneo husika na serikali isiwaingilie kwa kugawa ardhi kwa wawekezaji. walipendekeza pia uteuzi wa Jaji uwe unafanywa na Mwanasheria wa serikali sio Rais na Wakuu wa Mikoa na Wilaya wawe wanachaguliwa na wananchi wa maeneo yao.

Wakati huo abiria walikuwa wakisafiri na Treni hapo jana wamenusulika kifo baada ya Behewa moja lenye Namba 3366 kuacha njia.

Tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa 3:00 usiku muda mfupi baada ya Treni hiyo kuondoka katika kituo cha Mpanda kuelekea Tabora ajari hiyo ilitokea katika eneo la Tambukareli.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa