Home » » CHAGULAGA YAPIGWA MARUFUKU MLELE

CHAGULAGA YAPIGWA MARUFUKU MLELE



Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi yetu

Mkuu wa Wilaya mpya ya mlele mkoa wa Katavi Kanali Ngelema Lubinga amepiga marufuku mila zanazotumika na kabila la wasukuma za nichague mimi (Chagulaga) ili kupunguza ukimwi na mimba za wanafunzi.
Agizo hili amelitoa hapo jana kwenye mikutano miwili tofauti ya hadhara iliyofanyiika katika kata za mwamapili na usevya wilayani mlele.
Lubinga alitoa agizo hili kufuatia kupewa malalamiko ya kushamili kwa mila za chagulaga katika wilaya hiyo wakati wa shughuli za harusi na minada.
Alisema kuanzia sasa anaagiza askari wa jadi (sungusungu) kuhakikisha inawakamata wale wote wanaojishughulisha na chagulaga.
Wakamateni wanao vizia wasichama  wadogo wanao tembea mabarabarani kama mnavyowakamata waharifu wengine aliwaambia sungusungu.
Lubinga aliwataka watendaji wote wa vijiji kumpa orodha ya majina ya watu wanaowafahamu wanaojishughulisha na chagulaga huku akishangiliwa na wananchi.
Alieleza kuwa endapo hali hii itafumbiwa macho  upo uwezekano mkubwa wa kuzidi kuongezeka kwa ugonjwa hatari wa Ukimwi wilayani mlele.
Inashangaza mnawavamia waschana wadogo tuu waacheni  wasome shule kwani wanawake wenye umri mkubwa hamuwaoni aliwauliza Lubingu.
Alisema mila hizo za chagulaga zimesababisha baadhi ya wasichana ambao bado wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kutokana na kupewa mimba kwa kufanyishwa mapenzi bila hiari yao.
Kwa upande wake mkazi wa kata ya mwamapili Lupalika Utondo alisema kuwa wapo baadhi ya wazazi wa watoto wa kike wamekuwa wakifurahia watoto wao kufanyiwa mila hizo za kisukuma (chagulaga)
Aliliambia gazeti hili wazazi hao wamekuwa na imani ya watoto wao wakifanyiwa chagulaga ujue anabahati kwa kitendo hicho cha kugombewa wanaume wengi.
Nae Bonifasi Iddi alisema mila hizi za chagulaga zimekuwa  zikifanywa na kundi kubwa la vijana wa kisukuma ambai huwa wamekaa kwenye barabara huku wakisubili msichana apite na kisha  humfukuza mbio na kisha kuanza kumsombea kwa kumtamakia nichague mimi (chagulaga)
Hali hiyo inafikia wakati mwingine wao kwa wao vijana wa kiume huanza kupigana kwa fimbo ambazo huwa wamezishika mikononi mwao

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa