Home » » Shamba la Waziri Mkuu Pinda lawapa somo Madiwani Wilaya ya Mbinga.

Shamba la Waziri Mkuu Pinda lawapa somo Madiwani Wilaya ya Mbinga.


Na Walter Mguluchuma-Katavi yetu
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma wamepatiwa somo la ufugaji wa nyuki wa kisasa baada ya kutembelea katika shamba la waziri mkuu Mizengo Pinda lililopo kijiji cha kibaoni Katavi.
Madiwani hao wamelitembelea shamba la ufugaji nyuki hapo juzi wakati wa ziara yao ya siku mbili mkoani katavi kwa lengo la kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyopo mkoani katavi ili waweze kujifunza.
Msafar huo ambao pia ulikuwa na wataalamu mbalimbali wa halmashauri ya mbinga walikuwa wameongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Oddokilian Mwisho.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mbinga alisema wamefurahishwa na aina ya utaalamu wa kisasa wa ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ambayo wao walikuwa hawajawahi kuiona.
Nae mkuu wa mkoa wa katavi Dr. Rajabu Lutengwe aliwaeleza madiwani hao kuwa shamba hilo linamizinga ya kufugia nyuki ipatayo 200
Katika mizinga hiyo mzinga mmoja unauwezo wa kuvunwa lita 40 za asali kwa wakati mmoja kutokana na jinsi ilivyo tengenezwa kitaalamu.
Lutengwe aliwaeleza shamba hilo la ufugaji wa nyuki uvunaji wa nyuki hufanyika mara mbili kwa mwaka hali ambayo iliwafanya madiwani hao kuona ni kitu cha ajabu kutokana kushangazwa na uvunaji kufanyika mara mbili tofauti nao ambako hufanyika.
Alisema  ziara hiyo waliyoifanya itawasaidia zaidi halmashauri ya mbinga kutokana na halmashauri hiyo kuwa ni miongoni mwa halmashauri zenye kipato kikubwa hapa nchini.
Mbali na kutembelea shamba hilo la ufugaji wa nyuki la Pinda walitembelea mradi wa mashine ya kisasa ya ukoboaji wa Mpunga iliyoko katika kiijiji cha Mwamapuli tarafa ya mpimbwe kinacho andaliwa kuwa kituo cha kuuza mchere.
Mradi mwingine walio utembelea ni ujenzi wa kituo cha afya cha kiisasa cha tarafa ya Inyonga ambacho bado kinaendelea kujengwa ambapo mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya wilaya aya mpanda Godfrey Majuto aliwaeleza madiwani hao kuwa mpaka sasa umeisha gharimu shilingi milioni 600 na kikikamilika kitatumia zaidi ya shilingi milioni 800

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa