Home » » MAMA MJAZMZITO AFARIKI DUNIA AKIFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE TUMBONI

MAMA MJAZMZITO AFARIKI DUNIA AKIFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE TUMBONI


MJAMZITO AFARIKI DUNIA
  Na   Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwanamke mmojmjamzito aliyejulukana kwa jina la  Sesilia  John(39) Mkazi wa Kijiji cha Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi amefariki Dunia  baada ya kufanyiwa  upasuaji  wa uzazi  kufutia chelewa  kupatiwa huduma ya tatizo lililokuwa likimsumbua
Mjamzito huyo ambae alikuwa ni mkazi wa Kijiji cha Usevya alifariki hapo Desemba 2 katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako alikuwa amepelekwa kwa ajiri ya kupatiwa matibabu zaidi
Kaka wa marehemu huyo  Matheo  John  mkazi wa  mtaa wa Kotazi mjini Mpanda alisema  marehemu dada yake  alifariki Dunia  katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  baada ya kufanyiwa  opasuaji  ulitokana na uzazi
 Alisema Dada yake alikuwa anasubmbuliwa na ugonjwa wa kuumwa na tumbo  na alipokwenda  kwenye kituo cha afya cha Usevya  ambapo alipimwa na kuambiwa kuwa anatatizo la uvimbe tumboni   
 Matheo alieleza  baada ya  kuambiwa kuwa anatatizo la uvimbe aliandikiwa vidoge vya dawa kwa ajiri ya matibabu hayo  ambapo marehemu  alianza kutumia dawa hizo alizokuwa  ameandikiwa na mganga  wa  kituo cha afya hicho
 Alisema marehemu aliendelea kutumia dawa hizo lakini  hakupata nafuu yoyote hari ambayo ilimfanya arudi mara kwa mara kwenye kituo hicho cha afya ambapo waliendelea kumpatia dawa za kuondoa uvimbe tumboni
 Marehemu baada ya kuona  hari inazidi kuwa mbaya siku hadi siku licha ya  kuwa anatumia dawa  alizoandikiwa  ndugu  zake  waliamua  kumsafirisha  na kumpeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu zaidi
 Baada ya kufikishwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda alifanyiwa vipimo na kugundulika kuwa  ana ujauzito wa miezi mitano na mimba hiyo  imekaa nje ya mfuko wa uzazi
Alisema baada ya  vipimo hivyo  marehemu alidai kuwa anashangaa kuambiwa kuwa ni mjamzito wakati  yeye kwa kipindi hicho chote  amekuwa akipata siku zake kama kawaida
 Alieleza marehemu na  ndugu zake walikubaliana na   ushauri wa madaktari  wa  kumfanyia upasuaji marehemu na ndipo walipomfanyia upasuaji na kukuta  mimba hiyo imeisha oza kutokana na kutogunduliwa mapema kwa tatizo hili  na kupelekea kiumbe hicho kuharibika na kuoza
 Matheo  alisema  siku hiyo  baada ya kufanyiwa upasuaji huo  Marehemu  Sesilia  John  alifariki Dunia  na  mazishi yake yalifanyika katika makaburi ya Nsemlwa mjini  Mpanda Mkoani hapa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa