Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kanoge Makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilayani Mpanda Mkoa wakiwa na furaha za kukabidhiwa gari la wagonjwa kwa ajiri ya akina mama wajawazito na watoto lililotolewa na Serikali kwa ajiri ya kituo hicho
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Richald Mbogo akiwa katika gari la wagonjwa lililotolewa na Serikali kwa ajiri ya kituo cha afya Kanoge kwa ajiri ya kububea wajawazito na watoto wadogo gari hilo lilikabidhiwa jana na Mbunge huyo kwa Halmashauri ya Nsimbo Picha na Walter Mguluchuma
Na Walter Mguluchuma.
Katavi
Kituo cha Afya cha Kanoge Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda kimekabidhiwa gari maalumu la wagonjwa kwa ajiri ya kuwabebea akina Mama wajawazito na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ikiwa ni jitihada za Serikali za kuokoa uhai wa Mama na mtoto kufutia kituo hicho kuwa na tatizo kubwa la akina mama kujifungua kwa njia ya upasuaji.
Gari hilo aina ya Zuzuki lililotolewa na Serikali lilikabidhiwa juzi na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Richald Mbogo kwa mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kanoge Dk Adamu Mnyawe katika hafla iliyofanyika katika kituo hicho cha afya Kanoge na kuhudhuriwa na mamia ya wanachi waliokuwa wameongozwa na viongozi wa Halmashauri ya Nsimbo .
Akizungumza kabla ya kukabidhi gari hilo la wagonjwa Mbunge wa Jimbo hilo Richald Mbogo alisema viongozi wanatambua kero ambazo zinawakabil wananchi na ndio maana Serikali imetowa gari hilo .
Alisema kuw a Serikali imetowa gari hilo kwa kuwa inatambua mahitaji yanayohitajika kwenye kituo hicho cha afya na inaendelea kuboresha huduma za afya kwenye kituo hicho na ndio maana Serikali imetowa kiasi cha Tshs 400 ,000,000 kwenye kituo hicho kwa ajiri ya ujenzi wa wodi ya akina mama , chumba cha kuhifadhi maiti ,maabara na nyumba ya mganga .
Aliwataka waakikishe gari hilo wanalitunza vizuri na kulitumia kwenye makusudi yaliyokusudiwa na yeye kama Mbunge ataendelea kuwasemea Bungeni wananchi wa jimbo hilo juu ya kero za afya zinazowakabili .
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Afya Dk Adam Mnyawe alisema kituo hicho cha afya cha Kanoge kinakabiliwa na changamoto kubwa ya akina mama wajawazito kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida hari ambayo hulazimu kuwapatia rufa akina mama wajawazito kupekwa katika Hospital ya Manispaa ya Mpanda kutokana na kituo hicho kutokuwa na huduma za upasuaji .
Alifafanua kuwa kwa mwezi huwa wanapokea wajawazito kati ya 50 na 60 na wanaoshindwa kujifungua na kupewa rufaa ya kwenda katika Hospitali ya Manispaa huwa ni wajawazito kati ya 15 na 18 kwa kila mwezi ambapo usafirishwa kwa kutumia magari binafsi kutokana na kituo hicho hapo awali kutokuwa na gari hata moja .
Nae Agnes Nyamalila Mkazi wa Kaya ya Kanoge alisema akina mama wajawazito walikuwa wakipata shida sana ya usafiri pindi wanapokuwa wanashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida hari ambayo ilikuwa ikiwalazimu wasubilie usafiri wa magari yanayotoka Kata ya jirani ya Ugala kwa ajiri ya kumsafirisha mjamzito kwenda Hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Na kuna wakati magari hayo yalikuwa hayapiti hasa nyakati za usiku hari ambayo huwalazimu wanaume kuwabeba wagonjwa kwa kutumia machela.
Ndaisaba Jacksoni alieleza gari hilo la wagonjwa litawasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto na pia kuwapunguzia gharama walizokuwa wakizitumia ya fedha za kusafirishwa mjamzitokwani walikuwa wakitumia gharama kubwa ya kumsafirisha kutoka Kanoge hadi Hospitali ya Manispaa iliyoko umbali wa kilometa 30
0 comments:
Post a Comment