Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Mkazi wa Kijiji cha Songambele Kata ya Simbwesa Tarafa ya Karema Wilaya ya Tanganyika jina lake limehifadhi umri miaka 45 kwa sababu za kiuchunguzii kwa tuhuma za kumuua kikatili mke wak 5 akiwa anashudia tukio hil baada ya kutuhumu mke wake kuwa ni Malaya..
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema tukio la kupatikana kwa mwili wa marehemu huyo aliyekuwa amefukiwa ardhini baada ya kuuawa kikatili na mumewe lilitokea hapo juzi majira ya saa sita mchana katika Kijiji cha Songambele Kata ya Simbesa.
Alieleza kuwa marehemu huyo aliuawa na mumewe hapo januari 15 mwaka huu kwa kupigwa na mumewe kwa kutumia silaha za jadi fimbo na mpini wa jembe baada ya kumtuhumu kuwa anamausiano ya kimapenzi na wanaume wengine Kijijini hapo
Kamanda Nyanda alisema wakati muhumiwa huyo akitenda kitendo hicho ambacho kilishudiwa na mtoto wake mdogo wa kiume hadi baba yake alivyo muuawa mama yake na kisha kushimba shimo na kumfukia ardhini..
Baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa alirejea nyumbani kwake na kuendendelea na shughuli zake kama kawaida na alimtishia mtoto wake huyo mdogo na kumwambia asimwambie mtu yeyote.
Majirani waliokuwa wakimfahamu marehemu baada ya kuona haonekani Kijijini walianza kumuuliza mtuhumiwa mahali alipo mkewe nae alikuwa akiwaambia kuwa mkewe amesafiri .
Kamanda Nyanda alisema Jeshi la polisi lilipata taarifa ya mauaji ya mama huyo hapo machi 15 na ndipo lilipoanza uchunguzi wa tukio hilo la mauwaji ya kikatili .
Alileza baada ya kufanya uchunguzi ndipo hapo juzi waliweza kumtia mbaroni mtuhumiwa na baada ya mahojiano alikiri kufanya mauwaji hayo kwa kile alichodai kuwa alikasirishwa na tabia ya mke wake kuwa na wanaume wengine kijijini hapo na aliwaeleza polisi kuwa yuko tayari kwenda kuwaonyesha alipomfukia mke wake baada ya kumuua na kisha kuchimba shimo na kumfukia.
Baada ya mahojiano hayo hapo juzi majira ya saa sita mchana polisi walifika kwenye eneo ambalo mtuhumiwa alikuwa amemfukia marehemu mkewe na baada ya kufukua enee hilo walikuta mwili wa mkewe na waliweeza kuutowa na watu waliutambua kuwa ni mwili wa mke wa mtuhumiwa.
Kamanda Nyanda alieleza kuwa mwili wa marehemu baada ya kufukuliwa ulichukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Manispaa ya Mpanda .
Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika anatarajiwa kufikishwa Mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment