Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Wizara ya Maliasili na Utalii imeona umuhimu wa kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka mfumo wa kiraia na kuwa mfumo wa kijeshi kwani ulinzi wa rasilimali mistu unahitaji ukakamavu na weledi wa hali ya juu.
Hayo yalisemwa hapo jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya kijeshi kwa maafisa wandamizi 108 wa Wakala wa huduma za mistu TFS na wamamka ya uhifadhi wa Ngorongoro yaliofanyika kwa muda wa mwezi mmoja katika kituo cha Mafunzo cha Mlele Mkoani Katavi .
Mafunzo hayo yalikuwa ni maalumu kwa ajiri ya kuwaandaa na mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kutoka mfumo wa kiraia na kuwa mfumo wa kijeshi.
Hasunga alisema mapinduzi yanayoendelea katika sekta ya usafirishaji hususani matumizi ya usafiri wa pikipiki na kukuwa kw tennojia ya mawasiliano kumeongeza changamoto mpya katika kudhibiti uharifu wa mistu na wanyama .
Ni ukweli usiopingika kuwa kushamiri kwa uharibifu wa mazingira unaoendelea hapa nchini unatokana na sababu ya baadhi ya wananchi kufanya vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na kanuni za uhifadhi.
Alisema katika kukabiliana na uharibifu unaofanywa kwenye hifadhi za mistu na kukabilana na ujangili Wizara ya Maliasili na utalii ipo kwenye hatua ya mwisho ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kutoka kirai na kuwa wa kijeshi kwenye taasisi zote zilizopo chini ya Wizara hiyo .
Alifafanua kuwa bila mistu hakuwezi kuwepo na wanyama hivyo ni vema taasisi zote zinazofanya kazi ya uhifadhi wafanye kazi kwa kushirikiana ili kuweza kulinda rasrimali za nchi yetu .
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Llilian Matinga alisema Mkoa wa Katavi eneo lake zaidi ya asilimia 58 ni mapori ya akiba na Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Mtendaji Mkuu wa TFS Prof Dosantos Silayo alieleza kuwa hadi kufikia june mwaka huu wamepanga watumishi wao wapatao 500 wawe wamepatiwa mafunzo ya kijeshi katika kituo hicho cha mafunzo Mlele na mwezi ujao wamepanga kuwapatia mafunzo watumishi wao 150.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda alieleza kuwa Wilaya ya Mlele inakabiliwa na changamoto ya watu kujenga na kuishi ndani ya maeneo ya hifadhi za mistu na baadhi yao wameshindwa kuwaondoa kutokana na Serikali kuweka miundo mbinu kwenye maeneo hayo .
Alitaja baadhi ya miuondo mbinu iliyojengwa kwenye maeneo hayo ya ndani ya hifadhi za mistu kuwa ni majengo ya shule ofisi za Vjiji na nyumba za makazi ya watu .
Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Uzumbe Msindai aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo wahakikishe wanafanya kazi za uhifadhi wa mistu na wanyama kwa ufanisi mkubwa.
Nae Mkuu wa wapori ya akiba ya Rukwa, Lwafi Pascal Mhina alisema mapori hayo yanakabiliwa na changamoto ya ujangili wa mbao na hasa katika kipindi hiki cha masika kutokana na baadhi ya maeneo kutofika kutokana maeneo hayo kujaa maji .
Hata hivyo katika msako waliofanya hivi karibuni wameweza kukamata mbao zaidi ya 2600 na magogo 335 ambapo jumla ya watuhiwa 17 walikamatwa katika msako huo .
0 comments:
Post a Comment