WALTER MGULUCHUMA na IRENE TEMU
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
amependekeza shule ya msingi Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni aliyokuwa
ameijenga kupitia misaada ya wafadhi wakati akiwa madarakani kuwa kituo
cha afya kijijini hapo.
Mapendekezo hayo aliyatoa katika sherehe za
kuuaga mwaka 2017na kuukaribisha mwaka mpya 2018 zilizofanyika katika
Ukumbi wa Katavi Resort Mjini Mpanda zilizoandaliwana chama cha
waandishi wa Habari Mkoani Katavi kwa kushirikiana na baadhi ya wadau.
Lengo kubwa la kubadilisha matumizi ya
shule hiyo mpya ambayo haijawahi kutumika na imejengwa kisasa ni
kuchangia jitihada za serikali katika kuboresha huduma ya
afya Mkoani Katavi na Tanzania kwa ujumla na kupongeza jitihadi ambazo
serikali inaendelea kuzifanya katika kuboresha huduma hiyo.
Majengo hayo yanajumla ya vyumba vya
madarasa 26 ,nyumba za kuishi waalimu 24,nyumba ya utawala kubwa na
nzuri ,maktaba 2,eneo zuri la chumba cha kompyuta na kituo cha waalimu
kujifunzia hivyo endapo pendekezo hilo litapitiswa na serikali kituo
hicho kitaweza kupokea wauguzi toka mikoa mbalimbali ya nchi yetu.
Waziri mstaafu Pinda pia amepongeza huduma
za afya zinazotolewa na serikali katika kituo cha afya mamba kilichopo
katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi ambapo zaidi ya watu elfu 73 wanapatiwa
huduma katika kituo hicho kwa mwezi huku akina mama Zaidi ya 180
wakijifungua kwa njia salama na 10 hadi 15 wakifanyiwa upasuaji licha ya
kituo hicho cha afya kuwa na idadi ndogo ya watumishi.
Pia Pinda alizungumzia suala la uzazi wa mama na mtoto kuwa
hali bado hairidhishi na kuwataka viongozi waliopo serikali kuendelea
kutoa msukumo katika swala hilo la uzazi wa mama na watoto wachanga
kwani bado nguvu inahitajika hasa katika mikoa hii mipya
ambayo imekuwa ikipata ongezeko la watu kwa kasi kubwa na kutoa mfano wa
Mkoa wa Katavi kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 mkoa ulikuwa na zaidi
ya watu laki tano na 12 wakati kwa sasa hivi mkoa huo unakisiwa kuwa na
watu kati ya laki sita na laki saba
Kwa upande mwingine Waziri
Mstaafu amepongeza jitihada za serikali kupitisha mradi wa ujenzi wa
barabara ya lami kutoka Mkoani Tabora kwenda Mpanda ambao unatarajiwa
kuanza hivi karibuni na tayari makampuni matatu ya kichina
yameingia mkataba na serikali na kusisitiza mradi huo utapoanzaa
uwashirikishe wananchi wa maeneo hayon ili nao waweze kunufaika kupia
mradi huo bila kusahau mradi wa reli kuanzia Kaliua kwenda Karema.
Nae Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia
ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Liliani Matinga amepongeza hatua hiyo ya
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda kupendekeza shule hiyo kuwa chuo cha wauguzi kwani ni wazo zuri sana na kupongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali za kuletea wananchi maendeleo.
0 comments:
Post a Comment