Walter Mguluchuma Na Irene Temu
Wafanya biashara wa Manispaa ya Mpanda wanaofanya biashara za vibanda vya
maduka katika soko kuu la Manispaa ya Mpanda na Buzogwe wamesitisha kwa
siku nzima ya jana kufanya biashara na kuamua kufunga vibanda vyao kwa
kile wanachodai Manispaa ya Mpanda kuwa pandishia ushuru wa vibanda kutoka shilingi elfu kumi na tano hadi shilingi elfu 40,000.
Wakizungumza
na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wakiwa nje ya vibanda vyao
vilivyokuwa vimefungwa baadhi ya wafanyabiashara hao walisema hawako
tayari kuendelea kufanyabiashara kwenye masoko hayo mpaka hapo watakapo
pata suluhisho kati yao na Manispaa
Mmoja
wa wafanyabiashara katika soko la buzongwe Andrea Mashenene alisema
kuwa kiwango hicho walichipandishiwa kwa awamu moja ni kikubwa sana
ukilinganisha na faida wanazopata katika biashara zao
Alifafanua
kuwa hapo awali walikuwa wakilitozwa shilingi elfu kumi na tano kwa
mwezi na sasa wamepandishiwa kiwango na kutakiwa kulipa Tsh 40,000
kiwango ambachio ni kikubwa kwao
Alisema
hali hiyo inamlazimu yeye kufunga kibanda chake ambacho alilkuwa akiuza
viatu vya mitumba na kuangalia uwezekano wa kuhamishia biashara yake
kwenye meza zinazotumika kuuzia mboga mboga na matunda.
Naye mfanyabiashara wa soko kuu Josam Mateo akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake alifafanua kuwa kibanda kimoja kinatakiwa
kulipiwa ushuru wa Tshs 40,000 kwa mwezi kiwango ambacho kimekuwa ni
kikubwa kutokana na kodi mbalimbali wanazolipa kwenye eneo lao hilo la
biashara.
Alizitaja baadhi ya kodi hizo kuwa ni kodi ya Mapato TRA,leseni ya biashara inayotolewa na Manispaa,kodi ya mwenye kibanda,kodi ya zimzmoto na uokowaji na hiyo ya ushuru wa soko iliyopandishwa.
Nae
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Mkoa wa Katavi Amani Mahela
alisema kuwa swala hilo linapaswa kuzungumzwa kwa mezani na endapo
itashindikana kufanyika mazungumzo ni vema wafanyabiashara kwenda
Mahakamani na kuweka zuio la kuongezewa ushuru .
Alisema mikataba waliyopelekewa wafanyabiashara imekuwa na kasoro mbalimbali ambapo alitaja baadhi ya kasoro hizo
ni Mkurugenzi kuwa na mamlaka ya kunyang’anya kibanda kwa kutoa notisi
ya siku tisini pindi atakapokuwa anaona inafa kibanda hicho kuwa chini
ya Manispaa bila kujali mfanyabiashara huyo kama ana mikopo katika
taasisi mbalimbali za kibenki.
Diwani
wa kata ya kashaulili John Matongo yaplipo masoko hayo alisema
wafanyabiashara hao wamekuwa wakifanya biashara zao kwa mazoea hivyo ni
vyema kiwango hichi kilichoongezewa wakakilipa kama kilivyopangwa.
Alisema
wapo baadhi yao wamekuwa wakitumia siasa ilim watu waone kuwa
wafanyabiashara hao kuwa wameonewa kitu ambacho sio kweli kwani jambo
hilo lilianzia kwa wataalam wa Manispaa ambao hapo awali walipendekeza
kiwango kiwe Tshs 120,000 kwa mwezi lakini baada ya kushauriwa
namadiwani na kwenye kikao cha wawalikilshi wa wafanyabiashara
walikubaliana kishuke na kuwa Tshs 40,000 kwa mwezi na baadhi yao
walikuwa wamesha anza kulipa
MKurugenzi
wa Manisapaa ya Mpanda Michael Nzyungu alipopigiwa simu yake ya
kiganjani ili atoe ufafanuzi wa jambo hili iliita bila kupokelewa
Nae
Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo alisema kuwa swala hilo bado
lipo mikononi mwa wataalam wa manispaa litakapokuwa limeshindikana ndipo
litakapofikishwa kwao madiwani.
0 comments:
Post a Comment