Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Idadi ya makosa ya jinai yaliopipotiwa Mkoani Katavi kwa kipindi cha Mwaka 2017 yamepungua kutoka matukio 7549 yaliolipotiwa kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi kufikia matukio 7,150 na kuwa na upungufu wa matukio 399 sawa na asilimia 5.3 ya matukio yote .
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda mbele ya wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wa Mkoa huu wakati akisoma taarifa ya matukio yaliotokea katika Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha mwaka mmoja cha kuanzia mwezi . Januari 2017 hadi Desemba .
Kamanda Nyanda alisema matukio ya jinai yaliolipotiwa kwa kipindi cha januari hadi desemba 2017 yalikuwa ni 7,150 ikilinganishwa na matukio 7,549 yaliolipotiwa kwa kipindi cha mwezi januari 2016 na kuwa na upungufu wa matukio 399 sawa na asilimia 5.3 ya matukio yote.
Matukio makubwa ya jinai yaliolipotiwa ni 901 ukilinganisha na matukio 973 yaliolipotiwa kwa mwaka 2016 yakiwa na upungufu wa matukio 72 sawa na asilimia 7.4 ya matukio yote .
Alifafanua kuwa silaha zilizosalimishwa kwa mwaka 2016 jumla ni 9 ambapo bunduki aina ya SMG ni 2 na Gobore ni 7 ambapo silaha zilizosalimishwa kwa kwa mwaka 2017 jumla ni 16 SMG zikiwa ni 5 na Gobore ni 11.
Aidha katika kutekeleza dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi jeshi la polisi Mkoa wa Katavi wameendelea kuboresha huduma ya usalama kwa Wananchi na wameweza kutembelea vijiji 177 vya Mkoa wa Katavi na kufanya vikao na wananchi kwa kusikiliza kero zao wananchi ,maoni na ushauri.
Kamanda Nyanda alisema Jeshi la polisi wamejipanga kuendelea kufanya misako na doria za miguu mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba ili kukabiliana na matukio ya uhalifu .
Na wanaendelea kufanya mikutano ya hadhara ya polisi jamii katika vitongoji 933 na mitaa yote ya Mkoa wa Katavi na pia kuwaelimisha watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment