Tuesday, January 2, 2018

WAZIRI MSTAAFU PINDA APENDEKEZA SHULE KUWA CHUO CHAWAUGUZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WALTER MGULUCHUMA na IRENE TEMU
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amependekeza shule ya msingi Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni aliyokuwa ameijenga kupitia misaada ya wafadhi wakati akiwa madarakani kuwa kituo cha afya kijijini hapo.
Mapendekezo hayo aliyatoa katika sherehe za kuuaga mwaka 2017na kuukaribisha mwaka mpya 2018 zilizofanyika katika Ukumbi wa Katavi Resort Mjini Mpanda zilizoandaliwana chama cha waandishi wa Habari Mkoani Katavi kwa kushirikiana na baadhi ya wadau.
Lengo kubwa la kubadilisha matumizi ya shule hiyo mpya ambayo haijawahi kutumika na imejengwa kisasa ni kuchangia jitihada za serikali katika kuboresha  huduma ya afya Mkoani Katavi na Tanzania kwa ujumla na kupongeza jitihadi ambazo serikali inaendelea kuzifanya katika kuboresha huduma hiyo.
Majengo hayo yanajumla ya vyumba vya madarasa 26 ,nyumba za kuishi waalimu 24,nyumba ya utawala kubwa na nzuri ,maktaba 2,eneo zuri la chumba cha kompyuta na kituo cha waalimu kujifunzia hivyo endapo pendekezo hilo litapitiswa na serikali kituo hicho kitaweza kupokea wauguzi toka mikoa mbalimbali ya nchi yetu.
Waziri mstaafu Pinda pia amepongeza huduma za afya zinazotolewa na serikali katika kituo cha afya mamba kilichopo katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi  ambapo zaidi ya watu elfu 73  wanapatiwa huduma katika kituo hicho kwa mwezi huku akina mama Zaidi ya 180 wakijifungua kwa njia salama na 10 hadi 15 wakifanyiwa upasuaji licha ya kituo hicho cha afya kuwa na idadi ndogo ya watumishi.
Pia Pinda alizungumzia suala la uzazi wa mama na mtoto  kuwa hali bado hairidhishi na kuwataka viongozi waliopo serikali kuendelea kutoa msukumo katika swala hilo la uzazi wa mama na watoto wachanga kwani bado nguvu inahitajika  hasa katika mikoa hii mipya ambayo imekuwa ikipata ongezeko la watu kwa kasi kubwa na kutoa mfano wa Mkoa wa Katavi kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 mkoa ulikuwa na zaidi ya watu laki tano na 12 wakati kwa sasa hivi mkoa huo unakisiwa kuwa na watu kati ya laki sita na laki saba
 Kwa upande mwingine Waziri Mstaafu amepongeza jitihada za serikali kupitisha mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mkoani Tabora kwenda Mpanda ambao unatarajiwa kuanza hivi  karibuni na tayari makampuni matatu ya kichina yameingia mkataba na serikali na kusisitiza mradi huo utapoanzaa uwashirikishe wananchi wa maeneo hayon ili nao waweze kunufaika kupia mradi huo  bila kusahau mradi wa reli kuanzia Kaliua kwenda Karema.
Nae Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Liliani Matinga amepongeza hatua hiyo ya Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda  kupendekeza shule hiyo kuwa chuo cha wauguzi kwani ni wazo zuri sana na kupongeza jitihada  zinazoendelea kufanywa na serikali za kuletea wananchi maendeleo.

No comments:

Post a Comment