Na Walter Mguluchuma,Nkasi
AGATHA Mwananyau (19) aliyekatiza masomo akiwa Kidato cha Nne baada ya kupewa ujauzito amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 300,000/-
Msichana huyo aliyekuwa akisoma Kidato cha Nne katika Shule ya Sekonadari Mkangale katika Mji wa Namanyere Wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa aliacha masomo baada ya kupewa ujauzito na Alfa Nestory (20) .
Mshtakiwa huyo alishindwa kulipa faini hiyo ambapo ameanza kutumikia adhabu hiyo.
Juzi aliitwa na upande wa mashtaka kutoa ushahidi katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira ambapo alitoa ushahidi wa uongo akisema kuwa aliyempatia ujauzito hakuwa mshtakiwa Nestory bali alikuwa”mmachinga’ aliyetokea Mbeya tofauti na maelezo yake ya awali .
Ndipo Mwendesha Mashataka , Hamimu Gwelo alipomshtaki kwa kutoa ushahidi wa uongo ambapo jana alifikishwa mahakamani hapo na aliposomewa mashtaka hayo alikiri kutenda kosa hilo .
Akitoa hukumu Hakimu Rugemalila alisema kuwa amezingatia utetezi wa mshtakiwa kuwa apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mtoto mchanga mwenye umri wa miezi nane .
Mwisho
Na Walter Mguluchuma . Katavi
ZAIDI ya waendesha pikipiki maarufu “bodaboda” 130 wanaotoa huduma ya usafiri katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamekula kiapo cha kuwalinda wasichana dhidi ya mimba na ndoa za utotoni .
Kiapo hicho waliapa mbele ya Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii , Wazee na Watoto , Dk Faustine Ngugulile jana mjini hapa ambaye alieleza kuwa mkoa wa Katavi unaongoza nchini kwa mimba za utotoni kwa asilimia 45 huku akiutaka uongozi wa mkoa uone namna ya kuisadia Serikali ili wasichana waweze kutimiza ndoto zao.
“Hawa waendesha bodaboda ni ajira kwani wapo baadhi yao wamejenga nyumba na kusomesha watoto wao kamwe wasionekane kama wahuni isopkuwa jamii iwape ushirikiano “ alisisitiza .
Bodaboda hao waliahidi mbele ya Naibu Waziri kuwa kwa kuwa pikipiki zao vimekuwa vikitumika kuwapeleka wasichana wengi wao wakiwa ni wanafunzi kwenye nyumba za kulala wageni.
Hivyo watahakikisha kuanzia sasa watakuwa wanatoa taarifa kwa wazazi , walezi na Jeshi la Polisi pindi watakapom baini msichana waliyembeba na kumpeleka kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa na umri mdogo .
Walisema wao binafsi watajizuia kufanya vitendo vya ukatili wa
kingono dhidi ya watoto katika sehemu yoyote ile watakapo kuwepo
kwamba wapo baadhi yao wamechangia mimba za utotoni kwa kuwashawishi wasichana kufanya nao ngono .
Walieleza kuwa ni aibu mkoa wao (Katavi) kuwa ni kinara wa mimba za utotoni nchini wakiahidi kuwa watahakikisha wanalipunguza tatizo hilo mkoani humo .
.Nae Mwenyekiti wa waendesha “Bodaboda”, Stephano Asalile alisema kabla ya kula kiapo hicho walipewa mafunzo
na maofisa mkoa Wa Katavi waliotoka Wizara ya Afya , Maendeleo ya
Jamii , Jinsia ,Wazee na Watoto jinsi ya kuwalinda watoto na kuzuia
mimba za utotoni .
“Matunda ya mafunzo hayo yameanza kuonekana kwani tayari tumesha toa tarifa Jeshi la Polisi ambapo wanaume kumi wameshakamatwa wakituhumiwa kufanya ngono na wasichana wenye umri mdogo “ alieleza
Mwendesha ‘bodaboda “ , Leonard Wilson wazazi wakashirikiana na wao kwani kumekuwepo na tabia ya wasichana wadogo kujiuza katika nyumba za starehe .
Mwisho
0 comments:
Post a Comment