Na Walter Mguluchuma.
Katavi.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu mkazi wa kijiji cha |Sibwesa kilichopo katika wilaya ya Tanganyika , Wilson John (34) ambae ni kinyozi wa nywele kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba .
Mtoto huyo alivamiwa na kubakwa na mshtakiwa wakati akiwa anaoga bafuni nyumbani kwao huku wazazi wao wakiwa sebuleni wakiangalia luniga huku akimtishia kumuua iwapo atamweleza mtu yeyote ..
Akisoma
hukumu hiyo , Hakimu wa Mahakama hiyo ,Chiganga Ntengwa alisema kuwa
mahakama imerishishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashataka
pasipo kutia shaka kuwa mshtakiwa alitenda uhalifu huo .
Aliieleza mahakama hiyo kuwa mtu yeyote anayetenda kitendo hicho kama alivyofanya mshtakiwa nakuwa amefanya kosa kinyume na Kifungu cha Sheria namba 130 (1)na (2)e Kifungu cha Sheria namba 131 (3) cha kanuni ya adhabu .
Katika shauri hilo upande wa mashtaka uliita mashahidi sita akiwemo mtoto mwenyewe huku mshtakiwa akina hana shahidi yeyote .
Hakimu Ntengwa alisema kuwa ushahdi uliomtia hatiani mshtakiwa ni uliotolewa na mtoto mwenyewe na uchunguzi wa kitabibu uliothibitisha bila kutia shaka kuwa alingiliwa kimwili na sehemu zake za siri kuharibiwa pia ushahidi uliotolewa na mama yake mzazi .
Awali Mwendesha Mashtaka , Mwanasheria wa Serikali , Fravian Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa
alitenda kosa hilo Septemba 24 , mwaka huu saa mbili na nusu usiku
nyumbani kwa mtoto huyo ambapo mshtakiwa alikuwa amepanga humo .
Aliongeza kuwa wakati mshtakiwa akifanya uhalifu huo wazazi wa mtoto huyo walikuwa wakianglia luninga sebeleni mwao .
Kwa mujibu wa Shiyo usiku huo wa tukio mtoto huyo alichukua ndoo ya maji na kwenda basfuni kuonga ambapo mshtakiwa alikuwa amejibanza karibu ya mlango wa bafu ambapo alimweleza mtoto huyo kuwa aingie bafuni kuoga kwamba nay eye (mshtakiwa ) ataingia najisaidia haja ndogo humo humo .
Ilielezwa kuwa mtoto huyo aliingia bafuni na kuanza koga ambapo mshtakiwa alimvamia na kuziba mdomo kisha akambaka huku akimtishia kumuua endapo atamwambia mtu yeyote .
Shiyo alidai mahamani hapo mtoto huyo alienda kulala na wenzake chumbani bila kuwafahamiasha wazazi wake yaliyomsibu ambapo usiku alisumbuliwa na maumivu makali kwenye sehemu zake za siri .
Ilielezwa kuwa alipozidiwa na
maumivu makali alimuomba mtoto mwenzake wa kike waliyekuwa wamelala nae
chumba kimoja aende kumita mama yao mzazi ambaye alipoingia alishtuka
kuona godoro alilolalia lilikuwa limelowa damu huku mtoto huyo akilia ,
ndipo alipomwadithia mama yake kila kitu na alimtaja mshtakiwa .
Hakimu
Chiganga Ntengwa kabla ya kusoma hukumu alitowa nafasi kwa
mshitakiwa kama anayosababu yoyote ya msingi ya kuishawishi
Mahakama iweze kumpunguzia adhabu.
Akijitetea
mshtakiwa alidai kuwa hakutenda kosa hilo isipokuwa mama mzazi wa mtoto
huyo amemsingizia kwa kuwa alimkatalia kulipa kmodi mpya ya chumba ya Sh 40,000 kwa mwezi ambapo koda ya awali ilikuwa Sh 20,000/-
Utetezi
huo ulipingwa vikali na mwanashelia wa Serikali ambae
aliiomba Mahakama itowe adhabu kali kwa mujibu wa sheria ili
iwe funzo kwenye jamii kwa watu wengine wenye tabia
kama hiyo na kwa kuzingatia kuwa vitendo vya ubakaji
vimekuwa vikitokea mara kwa mara Mkoani Katavi .
Baada
ya kuzisikiliza pande hizo mbili za mashitaka na utetezi
Hakimu Ntengwa alisoma hukumu na kusema mshitakiwa Wilison
John mahakama imemuhukumu kutumikia jela maisha yake yote
kuanzia jana na kama hakuridhika na hukumu hiyo anayonafasi
ya kuomba rufaa kwenye mahakama nyingine ya ngazi ya juu zaidi .
Hakimu
Ntengwa baada ya kusoma hukumu hiyo alimkabidhi Wilison nakala
ya hukumu ya kesi hiyo na alikwenda nayo gerezani.
0 comments:
Post a Comment