Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Afisa Mtendaji wa Kata ya Litapunga Tarafa ya Ndurumo Wilayani Mpanda Agustino Wangabo 53 Mkazi wa Mtaa wa Airtel Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda amejinyonga hadi kufa juu ya paa la nyumba yake kwa kutumia mkanda wake wasuluali kwa kisa cha kufofia deni.
Tukio hilo la kujinyonga kwa mtendaji huyo wa Kata lilitokea hapo jana majira ya saa saba mchana nyumbani kwake na Marehemu katika Mtaa wa Airtel Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa .
Diwani wa Kata ya Uwanja wa Ndege Stephano Asalile tukio akisimilia tukio hilo alisema marehemu kabla ya kuchukua umamuzi wake wa kujinyonga alikuwa akidaiwa na mtendaji mwenzake wa huko Katumba kiasi cha Tshs 1,600,000 ambazo alizichukua toka mwezi Agosti mwaka huu kwa lengo la kumuuzia pikipiki SANLG ambayo ilikuwa ni mali yake na marehemu Wangabo.
Alisema baada ya mauziano hayo ya pikipiki marehemu aliombwa na mteja wake aweze kumpatia kadi ya pikipiki hata hivyo hakufanya hivyo na aliomba apewe pikipiki hiyo kwa lengo la kwenda nyumbani kwake kuchukua kadi ya pikipiki ili aje amkabidhi mteja wake .
Asalile alieleza pamoja na marehemu kuwa amelipwa kiasi hicho cha fedha hakuweza kukabidhi pikipiki hiyo toka mwezi Agosti na badala yake alitafuta mteja mwingine na kumuuzia pikipiki hiyo na baada ya kuuza hakuweza kurejesha fedha alizokuwa amechukua kwa mteja wake wa awali .
Mtendaji mwenzake alianza kufanya jitihada za kudai arejeshewe fedha zake lakini marehemu aliendelea kumipiga kalenda mara kwa mara na dalili za kutorudishiwa fedha zake zilianza kuonekana .
Alisema hari hiyo ilimfanya achukue uamuzi wa kwenda kutowa taarifa polisi ndipo hapo jana Mteja huyo alikwenda akiwa na polisi nyumbani kwa marehemu kwa lengo la kufatilia haki yake wakati wakiwa karibu na nyumba ya marehemu walimuona akiwa barabarani huku akiwa anakula mandazi na alipowaona alitimua mbio na kukimbilia ndani ya nyumba yake .
Ndipo polisi alipoweza kutafuta uongozi wa Serikali ya Mtaa kwa lengo la kufanya upekuzi wa kumsaka ndani ya nyumba yake na walipoingia ndani ya chumba chake waliweza kumwona marehemu akiwa juu ya mtamba wa paa lake huku akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mkanda wake wa saluali.
Kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa tuko la kifo hicho cha mtendaji wa Kata ya Litapunga ambacho alisema kimetokana na marehemu kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suluali .
Mwili wa marehemu Agustino Wangabo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Manispaa ya mpanda kwa ajiri ya kufanyiwa uchunguzi .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment