Saturday, November 18, 2017

FUNDI KINYOZI JELA MAISHA KWA KOSA LA KUMBAKA MTOTO BAFUNI WAKATI AKIWA ANAOGA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma.
     Katavi.

MAHAKAMA  ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi  imemuhukumu mkazi wa kijiji cha |Sibwesa  kilichopo katika wilaya ya Tanganyika , Wilson John (34)  ambae ni kinyozi wa  nywele  kifungo cha maisha jela   kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba .
Mtoto huyo alivamiwa na kubakwa na mshtakiwa wakati akiwa anaoga bafuni  nyumbani kwao  huku wazazi wao wakiwa sebuleni wakiangalia luniga huku akimtishia kumuua iwapo atamweleza mtu yeyote ..
Akisoma hukumu hiyo , Hakimu wa Mahakama hiyo ,Chiganga Ntengwa alisema kuwa mahakama imerishishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashataka pasipo kutia shaka kuwa mshtakiwa alitenda uhalifu huo .
Aliieleza mahakama hiyo kuwa mtu yeyote anayetenda  kitendo hicho kama alivyofanya mshtakiwa  nakuwa amefanya kosa kinyume  na Kifungu cha Sheria namba 130 (1)na (2)e   Kifungu cha Sheria namba 131 (3) cha  kanuni ya adhabu .
Katika shauri hilo upande wa mashtaka uliita mashahidi sita akiwemo mtoto mwenyewe  huku mshtakiwa akina hana shahidi yeyote .
Hakimu Ntengwa alisema kuwa ushahdi uliomtia hatiani  mshtakiwa ni uliotolewa na mtoto  mwenyewe  na uchunguzi wa kitabibu  uliothibitisha bila kutia shaka kuwa alingiliwa  kimwili na sehemu zake za siri kuharibiwa  pia ushahidi uliotolewa na mama yake mzazi .
Awali Mwendesha Mashtaka , Mwanasheria wa Serikali , Fravian Shiyo  alidai mahakamani hapo kuwa  mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 24 , mwaka huu saa mbili na nusu usiku nyumbani kwa mtoto huyo ambapo mshtakiwa alikuwa amepanga humo .
Aliongeza kuwa wakati mshtakiwa akifanya uhalifu huo wazazi wa mtoto huyo walikuwa wakianglia luninga sebeleni mwao .
Kwa mujibu wa  Shiyo usiku huo wa tukio mtoto huyo alichukua  ndoo ya maji na kwenda basfuni kuonga ambapo mshtakiwa alikuwa amejibanza  karibu  ya mlango wa bafu  ambapo alimweleza mtoto huyo kuwa aingie bafuni kuoga kwamba nay eye (mshtakiwa ) ataingia  najisaidia haja ndogo  humo humo .
Ilielezwa kuwa mtoto huyo aliingia bafuni na kuanza koga  ambapo mshtakiwa alimvamia na kuziba mdomo  kisha akambaka huku akimtishia kumuua endapo atamwambia mtu yeyote .
Shiyo alidai mahamani hapo  mtoto huyo alienda kulala na wenzake chumbani bila kuwafahamiasha wazazi wake yaliyomsibu ambapo usiku  alisumbuliwa na maumivu makali kwenye sehemu zake za siri .
Ilielezwa kuwa  alipozidiwa  na maumivu makali alimuomba mtoto mwenzake wa kike waliyekuwa wamelala nae chumba kimoja  aende kumita mama yao mzazi ambaye alipoingia alishtuka kuona godoro alilolalia lilikuwa limelowa damu huku mtoto huyo akilia , ndipo alipomwadithia mama yake kila kitu na alimtaja mshtakiwa .
Hakimu  Chiganga  Ntengwa  kabla ya kusoma  hukumu  alitowa  nafasi kwa  mshitakiwa   kama   anayosababu  yoyote ya   msingi ya  kuishawishi  Mahakama iweze  kumpunguzia   adhabu.
Akijitetea mshtakiwa alidai kuwa hakutenda kosa hilo isipokuwa mama mzazi wa mtoto huyo amemsingizia kwa kuwa alimkatalia kulipa kmodi mpya ya chumba  ya Sh 40,000 kwa mwezi ambapo koda ya awali ilikuwa Sh 20,000/-
Utetezi  huo  ulipingwa  vikali na   mwanashelia wa  Serikali   ambae   aliiomba  Mahakama   itowe  adhabu   kali kwa mujibu wa   sheria  ili   iwe   funzo  kwenye   jamii  kwa   watu   wengine   wenye   tabia   kama   hiyo   na  kwa  kuzingatia  kuwa    vitendo vya   ubakaji  vimekuwa   vikitokea  mara kwa  mara   Mkoani   Katavi .
 Baada ya  kuzisikiliza  pande  hizo  mbili za  mashitaka  na  utetezi    Hakimu  Ntengwa  alisoma   hukumu  na  kusema      mshitakiwa   Wilison  John   mahakama   imemuhukumu kutumikia  jela   maisha yake yote kuanzia  jana  na  kama   hakuridhika na  hukumu  hiyo   anayonafasi ya   kuomba  rufaa  kwenye   mahakama   nyingine ya  ngazi ya juu zaidi .
Hakimu    Ntengwa  baada ya  kusoma  hukumu  hiyo  alimkabidhi   Wilison  nakala ya  hukumu ya  kesi   hiyo  na    alikwenda   nayo   gerezani.

No comments:

Post a Comment