Na Walter Mguluchuma .
Mwanamke mmoja Beatilis
Kangu (48) Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda
Mkoa wa Katavi amefariki Dunia muda mfupi baada ya kutowa
sadaka kwenye ibada ya Kigango chake cha
Makanyagio B
Tukio la kifo cha
mwanamke huyo ambae alikuwa ni muumini wa dhehebu la Romani catholic lilitokea hapo juzi majira ya saa moja na nusu asubuhi
katika Mtaa wa Makanyagio Mjini hapa .
Makamu Mwenyekiti wa
Kigango hicho Charles Kanyanda alieleza kuwa siku hiyo
marehemu huyo alifika kwenye ibada kwenye kigango hicho kama
ambavyo walivyofika siku hiyo waumini wengine
kwa ajiri ya kusari .
Alisema baada ya kufika
alikwenda kujiunga na wanakwaya wenzake wa kwaya ya Kigango cha
Makanyagio ambapo nae alikuwa ni miongoni mwa waimbaji wa
kwaya siku kwenye ibada iliyokuwa ikiongozwa
na Katikisita wa Kigango hicho Agustino Ntalwila .
Ibada hiyo iliendelea
kama kawaida na ndipo ilipofikia muda wa kutoa sadaka na
marehemu alikwenda kutoa sadaka kama kawaida na kisha kurudi
kwenye kwaya na kuendelea kuimba.
Baada ya mahubiri ya
Katekista Ntalwila ulifuata utaratibu wa utoaji sadaka ya shukurani na
ndipo marehemu alipoinuka alipokuwa amekaa na kwenda kutoa
sadaka ya shukurani na baada ya kutoa sadaka
hiyo alianguka chini ghafla.
Wanakwaya wenzake
walijaribu kumpa msaada hata hivyo hari yake iliendelea kuwa
mbaya na hatimaye alifariki Dunia muda mfupi na
kuacha mshituko mkubwa kwa waumini wa kigango hicho
.
0 comments:
Post a Comment