Imeandikwa na Pety Siyame, Mlele
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu mkazi wa kijiji
cha Usevya, Mwasha Shija (18) kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa
kosa la kumbaka kwa siku nne mfululizo na kumweka kinyumba, msichana
mwenye umri wa miaka 14.
Mshtakiwa huyo alihukumiwa kutumikia kifungo hicho na Hakimu wa
Mahakama hiyo, Teotimus Sawi baada ya kukiri kosa hilo. Hakimu Sawi
alisema Mahakama imelazimika kumpa adhabu kali licha ya kutoisumbua kwa
kukiri kwake kosa, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Hakimu Swai alisema licha ya kukiri kosa mahakamani hapo, mshtakiwa
alikuwa ametenda kosa kinyume na Kifungu 130 (1) (2) (e) na 131 (1),Sura
ya 16 ya Kanuni ya Adhabu. Awali, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa
Polisi, Bakari Hongoli alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo Juni 26, mwaka huu, saa saba mchana katika Kijiji cha
Usevya kilichopo katika Kata ya Kibaoni wilayani Mpanda
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment