Na Walter Mguluchuma .
Katavi yetu
Mtu mmoja amekufa hapo hapo na wengine 13 kujeruhiwa na kulazwa hospitalini baada ya basi lao walilokuwa wakisafirili kuacha njia na kisha kupinduka kufuatia mwendo kasi wa dereva wa basi hilo .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema ajali hiyo ilitokea hapo jana majira ya saa tano na nusu huko katika Kijiji cha Ikondamoyo Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda barabara ya Tabora kwenda Mpanda Mkoani Katavi .
Alimtaja marehemu aliyefariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Paulo Mussa Mkazi wa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Shinyanga alifariki hapo hapo baada ya ajari kutokea .
Kamanda Nyanda alisema ajari hiyo ililihusisha basi la Kampuni ya ARYS'S lenye Namba za usajiri T473 CCC aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Dereva anaeitwa Jushua Bebedictor 45 ambae alikimbia baada ya ajari hiyo .
Alieleza mara baada ya ajari hiyo majeruhi wote 13 walichukuliwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambako wanaendelea kupatiwa matibabu huku majeruhi wanne hari zao zikiwa sio nzuri .
Damas Nyanda alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo kilisababishwa na mwendo kasi wa dreva ambae gari lilimshinda kukata kukona kutokana na kuwa kwenye mwendo mkali na kuacha njia na kisha kupinduka .
Baada ya dereva kukimbia jeshi la polisi lilifanya msako wa kumsaka na waliweza kufanikiwa kumkamata na mpaka sasa wanaendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi na mara uchunguzi utakapo kuwa umekamilika atafikishwa mahakamani ili akajibu mashitaka yanayomkabili .
Kamanda Nyanda ametowa wito kwa madereva kuacha tabia ya kuendesha magari kwa mwendo kasi na wazingatie sheria za usalama barabarani .
0 comments:
Post a Comment