Tuesday, August 1, 2017

MWANAMKE AFARIKI IBADANI MARA BAADA YA KUTOWA SADAKA KANISANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



 
 Na   Walter    Mguluchuma .
      
Mwanamke  mmoja   Beatilis  Kangu  (48)   Mkazi wa   Mtaa  wa    Makanyagio   Manispaa ya   Mpanda    Mkoa wa   Katavi  amefariki   Dunia  muda  mfupi  baada ya kutowa   sadaka  kwenye    ibada ya  Kigango  chake  cha   Makanyagio    B
 
 Tukio  la  kifo cha  mwanamke huyo  ambae alikuwa ni muumini wa   dhehebu  la   Romani   catholic lilitokea  hapo juzi  majira ya saa moja  na  nusu   asubuhi  katika   Mtaa wa   Makanyagio   Mjini  hapa .
Makamu   Mwenyekiti wa   Kigango  hicho   Charles   Kanyanda   alieleza  kuwa  siku  hiyo  marehemu  huyo   alifika  kwenye   ibada kwenye   kigango  hicho  kama   ambavyo  walivyofika  siku  hiyo  waumini  wengine kwa  ajiri ya  kusari .
 
Alisema  baada ya  kufika   alikwenda  kujiunga  na   wanakwaya  wenzake wa  kwaya ya  Kigango cha   Makanyagio   ambapo  nae   alikuwa  ni  miongoni  mwa  waimbaji wa  kwaya  siku  kwenye  ibada iliyokuwa  ikiongozwa  na  Katikisita wa  Kigango  hicho    Agustino   Ntalwila .
  Ibada hiyo  iliendelea  kama  kawaida  na  ndipo  ilipofikia  muda wa kutoa  sadaka na  marehemu   alikwenda kutoa  sadaka  kama  kawaida  na  kisha  kurudi   kwenye   kwaya na kuendelea   kuimba.
Baada ya  mahubiri ya   Katekista   Ntalwila  ulifuata  utaratibu wa  utoaji   sadaka ya   shukurani  na  ndipo  marehemu  alipoinuka  alipokuwa   amekaa na  kwenda  kutoa   sadaka ya   shukurani  na  baada ya kutoa sadaka   hiyo   alianguka   chini  ghafla.
 
  Wanakwaya  wenzake  walijaribu  kumpa  msaada  hata  hivyo   hari  yake  iliendelea kuwa   mbaya  na  hatimaye   alifariki   Dunia     muda   mfupi  na kuacha mshituko  mkubwa kwa  waumini wa kigango  hicho .
 
Kanyanda   alisema  mazishi ya  marehemu   Beatilis  yalifanyika    katika   makaburi ya   Mwanga  na    misa ya     mazishi  iliongozwa na    Paroko wa   Kanisa  Katoliki   Parokia ya   Maria   Emakulata   Monsinyori  Padri   George   Kisapa .

No comments:

Post a Comment