Na Walter Mguluchuma .
Katavi.
Baraza la Wazee la Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi limetowa tamko la kumuunga mkono Rais John Magufuli katika jitihada zake za kupambana na watu wanao hujumu rasilimali za Nchi na wamelaani vikali mauwaji yaliotokea Kibiti na Mkulanga .
Tamko la Baraza la Wazee hao lilitolewa hapo jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga katika kikao cha Baraza la Wazee wa CCM wa Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa Maji mjini hapa .
Akisoma tamko hilo Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM wa Mkoa wa Katavi Thomas Ngozi alisema wao kama wazee wanamuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada kubwa anazofanya za kupambana na watu wanao hujumu raslimali za Nchi .
Alisema wamekaa na kuona Nchi inavyo kwenda hivyo wameona wamtie moyo Rais kutokana na kazi ngumu inayoifanya ya kuiongoza Nchi ya Tanzania na wanampongeza kwa kazi kubwa anayoifanya .
Mwenyekiti huyo alieleza kuwa wanatambua upendo mkubwa alionao Rais kwa Watanzania na hasa kwa kuwajari sana watu waliomaskini pasipo kuwabagua kutokana na umaskini walio nao watu .
Alisema wapo baadhi ya Watanzania wachache. Ambao wanamacho lakini wamekuwa wakijifanya kuwa wao hawaoni. Na wamekuwa wakitaka kukwamisha jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano .
Alieleza kuwa kama ni wizi umevuka mipaka na Serikali imekuwa ikiibiwa kwa kipindi kirefu hivyo Rais ameamua kupambana na wizi huo hivyo ni vema jitihada hizo anazozifanya zikaungwa mkono na watu wote bila kujali itikadi za vyama.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alisema Serikali ya Mkoa wa Katavi inaunga mkono jitihida kubwa ya Rai katika kumbana na vita ya watu wanao hujumu uchumi wa Nchi .
Alisema vita hii inahitaji Rais aungwe mkono kwani sio watu wote ambao wanaohifurahia licha kwa kipindi hiki kifupi mabadiliko yameonekana .
Mkuu huyo wa Mkoa aliwaahidi wazee hao kuwa salamu zao hizo atazifikisha kwa Rais haraka iwezekanavyo
0 comments:
Post a Comment