Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Serikali Mkoani Katavi imetowa onyo kuwa haitamfumbia macho mtu yeyote atakae onyesha nia ya kuhujumu vyama vya Ushirika kwani lengo la Serikali ya Mkoa ni kuendelea kusimamia ushirika imara na wenye nguvu ya kiuchumi kwa kuwahudumia wanachama wake kikamilifu /
Onyo hilo lilitolewa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga kwenye hotuba yake wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Ushirika Mkoa wa Katavi iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishina wa Polisi Paulo Chagonja uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji Mjini hapa .
Alisema Serikali Mkoani Katavi itaendelea kusimamia ushirika na haitamfumbia macho mtu yeyote atakae onyesha nia ya kuhujumu vyama vya Ushirika .
Lengo la Mkoa wa Katavi ni kuendelea kuwa kinara kwa kuwa na ushirika imara na wenye nguvu kiuchumi kwa kuwahudumia wanachama wake kikamilifu .
Alisema kumekuwa na malalamko kwa baadhi ya vyama vya ushirika yanayosababishwa na udhaifu katika uendeshwaji wa vyama vya ushirika na udhaifu huo umetokana na usimamizi hafifu, kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya viongozi na kukosekana kwa uwazi wa utoaji wa taarifa kwa wakati .
Alitowa rai kwa viongozi wa ushirika wa Mkoa huu kufanya kazi kwa bidii,waledi uaminifu na uadilifu katika utendaji kazi ili mapungufu hayo yalioonekana yasitokee tena .
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kilimo cha Tumbaku kimeanza kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupungua kwa soko au mahitaji kutoka kwa makampuni ya ununuzi na chamgamoto ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ambapo Serikali imeelekeza kuwa kila mkulima apande miti 150 katika shamba lake binafsi ,kutunza miti ya asili NIGITRI 200.
Naibu Mrajis vyama vya ushirika Tanzania Charles Malunde alieleza kuwa vyama vya ushirika vinaweza kufa au kupolomoka endapo viongozi wanao ongoza ushirika huo kuwa ni wabovu .
Naibu Mrajis aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo wa jukwaa la ushirika kuwa kila mkoa unachangamoto za ushirika wapo baadhi ya watu wakimbiwa ushirika wanajua umeisha kufa na wengine wanajua kuwa Sacos sio ushirika.
Nae Mrajis Msaidizi wa Vyama vya ushirika wa Mkoa wa Katavi Luhigiza Sesemkwa alisema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuingilia shughuli za vyama vya ushirika na kufanya maamuzi bila kuzingatia sheria na taratibu za ushirika .
Alifafanua mwamko mdogo kwa wananchi katika kujiunga na ushirika ikizingatia idadi ya wakazi wa Mkoa wa Katavi ni 671,194 ambapo wanachama wa ushirika ndani ya Mkoa ni 16,000 tuu ambayo ni sawa na asilimia 2.8 ya wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012.
Mwenyekiti wa chama cha Msingi Nsimbo Maganga Kasea alizilalamikia Halmashauri kwa kushindwa kutengeneza miundo mbinu ya barabara kwenye maeneo yanayo zalisha Zao la Tumbaku licha ya kuwa wanapata fedha nyingi zitokanazo na ushuru wa Tumbaku ambapo asilimia 5 ya thamani ya fedha za mauzo ya tumbaku huenda kwenye Halmashauri husika .
Katika uzinduzi wa jukwaa la ushirika Mkoani katavi wajumbe wa mkutano huo walimchagua Moses Kabeja kuwa Mwenyekiti wa jukwaa laa ushirika la Mkoa wa Katavi baada ya kuwashinda wagombea watano wa nafasi hiyo na Makamu Mwenyekiti alichaguliwa Suzana Kasera aliyewashinda wagombea wanne wa nafasi hiyo .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment