Na Walter Mguluchuma .
Katavi.
Katavi.
SHEIKH Hamisi Kikoti amenusurika kichapo kutoka kwa waumini wa
kikristo baada ya kutoa kauli ya maudhi dhidi yao wakati wa maziko ya
askari mgambo maarufu na aliyekuwa akiaminika na wananchi wa Kata nzima, Tano Nkuba .
Tafrani hiyo ilitokea hivi karibuni katika eneo la makuburi katika
kijiji cha Majalila kilichopo katika wilaya ya Tanganyika katika mkoa
wa Katavi ambapo waumini wa kikristo walisusa maziko ya askari
mgambo huyo na kuamua kurejea msibani
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Ntongwe kilichopo kijiji hicho cha
majalila , Frank Kibigazi alifanikiwa kuumaliza mgogoro huo baina ya
waumini wa madhehebu hayo mawili kufikia uamuzi wa kutoshirikiana
kwa lolote lile kijijini humo .
Akifafanua diwani huyo alieleza kuwa baada ya kuibuka kwa mgogoro huo
baina ya waumuni wa kikristo na wenzao wa kiisilamu aliwakutanisha
viongozi wao ambapo walikubalina kuwa wakikutana na waumini waokwenye
nyumba zao za ibada watawatangazia kuwa mgogoro huo umekwisha .
Mgogoro huo ulisababishwa na Sheikh Kikoti wakati alipokuwa akiongoza
ibada ya maziko ya askari mgambo wa kijiji hicho ambapo alitoa kauli
ambazo waumini wa kikristo walidai kuwa amewakashifu na kusababisha
vurugu kuibuka makaburini huku wakiristu wakitaka kumpiga.
.
Sheikh huyo anadaiwa kutowa kauli kuwa
waislamu ndugu zao ni waislamu na hivyo wasali sana wasiwe
kama wenye majina ya John ambao hawajuwi kusali na wanaabudu ovyo
ovyo.
Diwani huyo alieleza kuwa mgogoro huo alifanikiwa
kuumaliza kwa kushirikiana pia na baadhi ya wazee wa
Kijiji hicho.
Mwalimu wa Dini wa Kanisa katoliki kijijini humo , Credo Lusambo
aliingilia kati na kuwasihii waumuni wake wapunguze jazba lakini hata
walipomwomba Sheikh Kikoti kuwaomba radhi alikataa mpaka diwani
Kibigazi alipoingilia kati na kuwakutanisha viongozi wa dini wa pande
hizo mbili .
0 comments:
Post a Comment