Na Walter Mguluchuma
Katavi
Diwani
wa Kata ya Ntongwe Wilaya ya Tanganyika Mkoa
wa Katavi Frenk Kibigazi jana amefanikiwa kuutatua mgogoro wa
kidini baina ya wakristu na Waislamu wa Kijiji cha Majalila
uliokusababisha Sheikh Hamis Kakoti kunusurika kipigo kutokana na kauli
aliyoitoa wakati wa mazishi ya mwislam ambayo ilitafsiriwa kuwa ni
kejeli kwa wakristu.
Mgogoro huo ulitokea wakati wa mazishi ya baina ya waumini mazishi ya mgambo aliyekuwa anaaminika na wakazi
wa Kata hiyo Tano Nkuba ambae mazishi yake yalikuwa
yalifanyika siku hiyo ambapo sheikh huyo alipokuwa akiwaasa waislamu
aliwaambia kuwa "wasali sana wasiwe kama wakina John na Katabi ambao
wanaabudu tu" kauli iliyowakwaza wakristu.
Baada ya kauli hiyo lilizuka zogo kubwa
makaburini hapo hadi pale Katekista wa dhehebu la
Katoliki Credo Lusambo alipoingilia kati na kuwasihi waumini wa
kikristu wapunguze hasira na kuwaahidi kuwa
na swala hilo litakwenda kumaliziwa kwenye msiba nyumbani kwa marehemu.
Walipo fika
nyumbani kwa marehemu waumini wa dini ya Kikristu walidai kuwa
kuanzia siku hiyo hawako tayari tena kushirikiana
na Waislamu mpaka hapo Shekhe Kakoti atakapo waomba radhi kwani
lugha aliyoitumia ilikuwa ni ya kuwakashifu wakristu na imewaudhi
kupita kiasi.
Hata hivyo Shekhe
huyo hakukubali kuomba msamaha kutokana na kauli yake
aliyoitoa hari ambayo iliwafanya wakristu waondoke msibani hapo huku wakiwa na msimamo wa kutoshirikiana na waislamu kwa jambo lolote lile liwe zuri ama baya.
Baada
ya siku kadhaa kupita ndipo diwani wa Kata ya Ntongwe, Frenk
Kibigazi alisema haiwezekani mgogoro huo ukaachwa uendelee kuwa ulivyo
hali iliyo mlazimu kuitisha mkutano ambapo
alishirikisha pande mbili hizo ili kutatua mgogoro huo wa kidini uliokuwa umetokea siku kadhaa zilizopita.
Katika
mkutano huo diwani huyo alisema kuwa yeye kama kiongozi wa kata hiyo
hayupo tayari kuona kunamgawanyiko na watu wakiishi bila kushirikiana
kitendo ambacho ni kibaya na sio utamaduni wa kitanzania kwani
watanzania panapotokea jambo daima wamekuwa wakikutana na kulitatua ili
maisha ya amani, mshikamano na ushirikiano yaendelee kama awali.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu viongozi hao
wa dini walikubaliana kumaliza tofauti zao na kukubaliana pia
kwenda kwa waumini wao makanisani na misikitini kuwaeleza
kuwa mgogoro uliokuwepo umekwisha hivyo waendelee kushirikiana kwenye mazishi
na kwenye mambo mengine kama kawaida na kuwaonya viongozi wa kidini
kujiepusha na kauli zinazoweza kukwaza upande mwingine kwani daima
zimekuwa ni chanzo cha mifarakano katika maeneo mengi ndani na nje ya
nchi yetu.
0 comments:
Post a Comment