Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda ametangaza kuwa amemteua Aliyekuwa mkuu wa polisi mstaafu wa Wilaya ya Mpanda OCD Zeno Malesa kuwa mshauri wa maswala ya ulinzi na usalama wa Mtaa wa Kasimba katika Manispaa ya Mpanda kutokana na juhudi zake alizozifanya za kupunguza uharifu na matukio ya kujamiana kabla ya kustaafu kwake kazi katika jeshi la polisi .
Uamuzi huo wa kumteua Malesa kuwa mshauri wa jeshi la polisi katika maswala ya ulinzi na usalama katika mtaa huo uliotolewa hapo jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi wakati wa sherehe za kumuaga OCD huyo mstaafu zilizofanyika katika ukumbi wa Neema uliko katika Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda .
Alisema OCD huyo mstaafu amelitumikia jeshi la polisi kwa uaminifu mkubwa kuanzia mwaka 1973 alipojiunga na jeshi hilo hadi Julai 1 mwaka huu ambapo ameweza kufanya kazi ya polisi kwa kipindi cha miaka 44 kwa uadilifu mkubwa .
Alifafanua kuwa kwa kipindi alichoongoza Wilaya ya Mpanda amefanya kazi nyingi mbalimbali za kupambana na uharifu na ameweza kupunguza matukio ya ualifu kwa kiasi kikubwa sana .
Pia ameweza kupunguza matukio ya kujamiana kutoka matukio kumi kwa kipindi cha mwaka jana hadi kufikia matukio matatu kwa kipindi cha mwaka huu wa 2017.
Nyanda alieleza kuwa kutokana na mchango wake huu mkubwa katika jeshi la polisi ndio maana ameamua kumteuwa kuwa mshauri wa maswala ya ulinzi na usalama katika mtaa anao ishi wa Kasimba iliaendelee kutowa mchango wake kwa jeshi la polis i
Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishina wa Polisi Paulo Chagonja alisema kuwa jeshi la polisi linajivunia mafanikio ya OCD huyo mstaafu na atakuwa ni daraja kati ya polisi na Raia na Balozi .
Alisema ukiona mtumishi wa jeshi la polisi ameweza kufanya kazi na kufikia ngazi aliyokuwa nayo Malesa ujuwe kuwa mtu huyo alikuwa ni mwadilifu na ndio maana jeshi la polisi lilimwamini .
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama wa Wilaya ya Mpanda ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga alisema kuwa hari ya matukio ya uharifu kwa wilaya ya Mpanda yamepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano ulipo baina ya polisi na wananchi hivyo alimtaka ocd alihamishiwa kwenye Wilaya hiyo kuendeleza ushirikiano na mahusiano na wananchi kama yalikuwepo .
0 comments:
Post a Comment