Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wizara ya Maliasili na utalii imepiga marufuku kwa watumishi wote waliochini ya Wizara hiyo kutojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya wala kufanya biashara hiyo kwani ni kufanya hivyo ni kuitia aibu Wizara hiyo na Serikali.
Agizo hilo lilitolewa hapo jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya Wahifadhi 98 wa wanyama pori TAWA na TANAPA mmoja yalifanyika katika kituo cha mafunzo cha Mlele Mkoani Katavi .
Alisema ni marufuku kwa mtumishi yoyote aliyechini ya Wizara hiyo kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya au kufanya biashara hiyo kwani ni aibu kwa Wizara na Serikali na endapo mtumishi atakae bainika atachukuliwa hatua kali .
Meja Jenerali Milanzi alieleza Askari wa Hifadhi wa wanyama pori wanapokuwa wanafanya kazi zao maporini pindi wanapo ona mashamba ya bhangi wasijiingize kuvuta na badala yake wawe wanatowa taarifa kwa mamlaka husika .
Alifafanua kuwa kwa sasa hari ya ujangili imepungua hapa nchini hata hivyo juhudi za kupambana na ujangili bado zinaendelea kwani hakuna sababu za kuridhika kwani ujangili bado upo .
Alisema Wizara yake inaendelea kuweka mipaka kwenye Hifadhi zote ili kuondoa migogoro ya mipaka na wananchi ambao wamekuwa wakivamia maeneo ya Hifadhi kwa kisingizio cha kutojua mipaka .
Aliwataka Askari wa Hifadhi za Wanyama pori kutotumia nguvu kubwa mahari ambapo apasitahili wala kuuwa watu kwani Serikali haipendi kuona watu wake wanakufa .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mam
laka ya usimamizi Wanyama pori Tanzania TAWA Martin Loibooki alisema TAWA imeanza kuwaandaa watumishi wake kujiandaa kuingia kwenye mfumo wa Jeshi Usu ili kuboresha ulinzi wa rasilimali za maliasili kwa ujumla .
Alisema imefikia wakati wa kulazimika kutoka kwenye mfumo wa kiraia na kuingia kwenye mfumo wa jeshi usu kutokana na changamoto zilizopo zilizopo kwa sasa kwani majangili hawana lebo usoni .
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Mtango Mtahiko aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo wayatumie mafunzo hayo waliopata kwa vitendo
MWISHO
0 comments:
Post a Comment