Na Walter Mguluchuma.
Katavi
Mkazi wa Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda Godfrey Ediga ameshikwa na butwaa wakati akiwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda baada ya Mahakama hiyo kumwachia huru kutokana na kesi yake ya tuhuma za ubakaji iliyokuwa ikimkabili kukosa ushahidi wa kumtia hatiani .
Katika tukio hilo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odilo Amwol alisoma hukumu ya kumwachia huru mtuhumiwa huyo baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatia hatiani kwa kosa la tuhuma zilizokuwa zikimkabili za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16.
Pamoja na Hakimu Amwol kusoma huku ya kumwachia huru mtuhumiwa hakuamini kile ambacho kilichokuwa kimetokea na kubaki amesimama kizimbani licha ya kuambiwa aondoke hakuondoka hadi alipotolewa na Askari mmoja wa Polisi .
Awali katika kesi hiyo mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Michael Peter alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo hapo June 9 mwaka jana numbani kwao na msichana huyo .
Alisema siku hiyo ya tukio Godfery alifika nyumbani kwao na msichana huyo na kumwambia ameagizwa na baba yake ampatie supana ya kutengenezea baiskeili na ndipo aliidaiwa alimfata ndani na kumbaka .
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi Amwol alieleza kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha ushahidi wa kumtia mtuhumiwa hatiana kutokana na ushahidi walioutowa.
Miongoni mwa ushahidi uliotolewa kwenye kesi hiyo ni wakidaktari ambapo ulionyesha kuwa msichana huyo alikuwa haja ingiliwa kimwili katika sehemu zake za siri
0 comments:
Post a Comment