Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
A skari wa mamlaka ya Hifadhi ya wanyama pori
TAWA na TANAPA wakipita mbele ya mgeni rasmi katibu Mkuu wa
Wizara ya Maasili na utalii Meja Generali Gaudence
Milanzi ambae hayupo pichani wakati wa kufunga mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa ukakamavu kwa ajiri ya kujiandaa na kuelekea
jeshi usu mafunzo hayo yalifungwa jana katika kituo cha mlele .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na na
Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi akipokea heshima ya
gwaride kutoka kwa Askari wa TANAPA na TAWA wakati alikuwa
akifunga mafunzo ya wahifadhi wa daraja la pili yaliofanyika
jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele Mkoani Katavi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja
Generali Gaudence Milanzi akipeana mkono na mmoja wa Askari wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyama pori wa TAWA wakati alipokuwa
akifunga mafunzo ya Askari wa kutoka TANAPA na TAWA yenye lengo
ya kuwaanda kuingia kwenye mfumo wa jeshi usu yalikuwa yakifanika
katika kituo cha mafunzo cha Mlele Mkoa wa Katavi .
PICHA
NA Walter Mguluchuma.
Na Walter Mguluchuma Katavi
Mamlaka ya Hifadhi ya wanyama Tanzania itaendelea kushirikiana na TANAPA na NCAA vyombo vya usalama ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kiuhifadhi na imeanza kujiandaa kiutendaji kazi wa kutoka kwenye mfumo wa kiraia na kuwa jeshi ili kukabiliana na hari ya ujangili hapa Nchini.
Kauli hiyo hiyo ilitolewa hapo jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi Wanyama pori Tanzania TAWA Martin Loibook i wakati wa kufunga mafunzo ya ukakamavu kwa wahifadhi Wanyama pori wa TAWA na TANAPA katika kituo cha Mlele Mkoani Katavi mafumbo ambayo yalifungwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi .
Alisema mamlaka itaendelea kutoa mafunzo ya uteyari wa watumishi wake wa kupokea mabadiliko ya kuelekea katika mfumo wa jeshi usu ilikukabiliana na changamoto zilizopo sasa .
Alizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni uvamizi wa mifugo katika maeneo ya Hifadhi ,migogoro ya mipaka na kuingizwa nchini kwa silaha za kivita zinazotumika kufanya ujangili .
Pia kurudishwa kwa baadhi ya vitalu vya uwindaji wa kitalii pamoja na uwelewa mdogo wa wananchi katika kuunga mkono uhifadhi wa rasilimali za maliasili .
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA ABLAHAMU Kaniki alisema Bodi ya Usimamizi Wanyama pori TAWA inafuatilia kwa karibu matayarisho yanayofanywa ya kuwaandaa watumishi kuingia kwenye mfumo wa jeshi Usu ili kuboresha ulinzi wa rasilimali kwa ujumla .
Alifafanua Bodi imeisha baini kwamba ofisi nyingi za wakuu wa mapori ya akiba zipo mbali na maeneo wanayoyasimamia na wengi wanaishi mijini jambo hilo halikabaliki kwani linadhofisha ulinzi wa rasilimali hivyo Bodi ime wameagiza wakuu wote wa mapori ya akiba kuhamia jirani na mapori ya akiba .
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudenci Milanzi alisema Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea na hatua za kuanzisha mfumo wa jeshi usu katika sekta za wanyama pori na mistu .
Hivyo mpango wa kutowa mafunzo ya ukakamavu ni maandalizi ya awali kuelekea katika mfumo huo na mafunzo hayo ni endelevu na yatatolewa kwa watumishi wote wanaohusika na ulinzi wa rasilimali za maliasili , katika sekta za wanyama na mistu .
Alisema Wizara inaamini kwamba changamoto za ujangili na uvunaji haramu wa mistu na matatizo mbalimbali yanayoikakabili uhifadhi nchini hayawezi kutatuliwa kwa mfumo wa utendaji kazi wa sasa wa kiraia
Hivyo Wizara inakamilisha taratibu za kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka wa kiraia kwenda jeshi usu mabadiliko haya ya kimfumo ni matakwa ya sheria ya uhifadhi wanyama poti Na 5 ya mwaka 2009 ambayo imeanisha kwamba kutaundwa kikosi cha jeshi usu ili kuhakikisha ulinzi kamili wa rasilimali katika maeneo yaliohifadhiwa .
0 comments:
Post a Comment