Monday, March 13, 2017

MAMLAKA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI TANZANIA ITAENDELEA SHIRIKIANA NA TANAPA na NCAA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UHIFADHI WA WANYAMAPORI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 A skari wa     mamlaka ya  Hifadhi ya   wanyama  pori   TAWA  na  TANAPA  wakipita  mbele ya    mgeni  rasmi  katibu  Mkuu  wa   Wizara  ya  Maasili na   utalii   Meja   Generali   Gaudence   Milanzi   ambae  hayupo   pichani  wakati wa  kufunga  mafunzo ya kuwajengea uwezo wa  ukakamavu kwa  ajiri ya kujiandaa na  kuelekea    jeshi usu  mafunzo  hayo  yalifungwa  jana  katika  kituo cha     mlele .
 Katibu  Mkuu  wa  Wizara ya    Maliasili na  na  Utalii  Meja  Generali  Gaudence  Milanzi  akipokea  heshima   ya  gwaride  kutoka     kwa   Askari wa  TANAPA  na  TAWA  wakati  alikuwa  akifunga  mafunzo ya  wahifadhi wa   daraja  la pili  yaliofanyika  jana  katika  kituo cha   mafunzo  cha  Mlele  Mkoani   Katavi.
Katibu  Mkuu wa  Wizara ya  Maliasili na  Utalii Meja   Generali  Gaudence  Milanzi   akipeana  mkono  na  mmoja wa   Askari wa  Mamlaka  ya   Hifadhi ya   Wanyama  pori  wa TAWA  wakati  alipokuwa  akifunga  mafunzo ya  Askari wa  kutoka   TANAPA  na  TAWA  yenye  lengo ya  kuwaanda kuingia kwenye  mfumo wa jeshi  usu  yalikuwa  yakifanika  katika  kituo cha  mafunzo  cha Mlele  Mkoa wa  Katavi .
   PICHA  NA  Walter  Mguluchuma.
Na  Walter  Mguluchuma Katavi

  

Mamlaka ya   Hifadhi ya   wanyama   Tanzania   itaendelea  kushirikiana  na   TANAPA  na   NCAA   vyombo    vya  usalama  ili  kutafuta   ufumbuzi  wa   changamoto  za  kiuhifadhi  na imeanza kujiandaa  kiutendaji  kazi  wa kutoka  kwenye  mfumo wa  kiraia na  kuwa   jeshi    ili  kukabiliana  na  hari ya  ujangili  hapa   Nchini.


Kauli  hiyo    hiyo   ilitolewa  hapo  jana  na     Mkurugenzi    Mkuu wa    Mamlaka  ya  usimamizi    Wanyama  pori   Tanzania  TAWA   Martin  Loibook i wakati wa  kufunga  mafunzo  ya  ukakamavu  kwa  wahifadhi   Wanyama  pori    wa  TAWA  na  TANAPA   katika  kituo  cha  Mlele   Mkoani  Katavi   mafumbo   ambayo yalifungwa  na   Katibu  Mkuu  wa  Wizara  ya   Maliasili na   Utalii    Meja   Generali    Gaudence  Milanzi .


Alisema   mamlaka   itaendelea  kutoa  mafunzo  ya  uteyari  wa  watumishi wake  wa  kupokea   mabadiliko  ya kuelekea   katika   mfumo wa   jeshi  usu  ilikukabiliana  na   changamoto  zilizopo  sasa .


 Alizitaja  baadhi ya    changamoto   wanazokabiliana  nazo  kuwa ni   uvamizi wa  mifugo  katika  maeneo ya   Hifadhi ,migogoro  ya  mipaka  na  kuingizwa   nchini  kwa  silaha  za   kivita   zinazotumika  kufanya     ujangili .


Pia  kurudishwa  kwa    baadhi ya   vitalu   vya   uwindaji  wa kitalii   pamoja na  uwelewa  mdogo  wa  wananchi   katika  kuunga  mkono   uhifadhi  wa  rasilimali   za   maliasili .

Mwakilishi wa Mwenyekiti  wa   Bodi ya   TAWA  ABLAHAMU  Kaniki   alisema    Bodi ya   Usimamizi   Wanyama  pori   TAWA   inafuatilia  kwa  karibu   matayarisho    yanayofanywa  ya  kuwaandaa  watumishi  kuingia  kwenye  mfumo wa  jeshi Usu  ili   kuboresha  ulinzi wa  rasilimali  kwa  ujumla .


Alifafanua   Bodi  imeisha  baini   kwamba   ofisi  nyingi   za wakuu  wa  mapori  ya  akiba   zipo   mbali na  maeneo  wanayoyasimamia  na  wengi  wanaishi   mijini   jambo  hilo  halikabaliki  kwani  linadhofisha   ulinzi  wa   rasilimali   hivyo   Bodi   ime    wameagiza wakuu  wote wa   mapori ya  akiba   kuhamia  jirani na  mapori ya   akiba .

Nae   Katibu   Mkuu  wa  Wizara  ya   Maliasili na   Utalii    Meja   Generali   Gaudenci   Milanzi   alisema   Wizara   ya  Maliasili na Utalii    itaendelea   na  hatua za kuanzisha   mfumo wa  jeshi usu   katika  sekta  za   wanyama  pori na  mistu .


  Hivyo  mpango wa  kutowa  mafunzo  ya  ukakamavu  ni  maandalizi ya   awali  kuelekea   katika  mfumo huo  na  mafunzo   hayo   ni   endelevu  na   yatatolewa   kwa  watumishi  wote   wanaohusika  na  ulinzi  wa  rasilimali  za  maliasili , katika  sekta za   wanyama    na  mistu .


Alisema   Wizara  inaamini   kwamba    changamoto  za  ujangili  na   uvunaji   haramu  wa  mistu  na   matatizo  mbalimbali  yanayoikakabili   uhifadhi   nchini   hayawezi  kutatuliwa  kwa  mfumo  wa  utendaji kazi wa  sasa  wa kiraia

Hivyo  Wizara   inakamilisha     taratibu   za   kubadili   mfumo   wa  utendaji  kazi    kutoka  wa   kiraia   kwenda  jeshi usu   mabadiliko   haya ya kimfumo ni  matakwa  ya   sheria ya   uhifadhi   wanyama  poti   Na  5 ya  mwaka  2009  ambayo  imeanisha   kwamba    kutaundwa   kikosi cha  jeshi usu  ili  kuhakikisha  ulinzi kamili   wa  rasilimali   katika  maeneo yaliohifadhiwa .


No comments:

Post a Comment