Walter Mguluchuma .
Katavi .
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Katika Wilaya Mpya ya Mkoani Katavi imepanga kua .
na Utalii wa Asili ili kuweza kuwavutia watalii mbalimbali wa nje ya Nchi na ndani ya Nchi na kuwaongezea wananchi kipato chao .
Hayo yalisemwa hapo juzi na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando wakati alipokuwa akiwa wahutubia wananchi wa Kijiji cha Vikonge Tarafa ya Kabungu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini hapo .
Alisema Wilaya ya Tanganyika inaomstu mkubwa wa Tongwe ambao upo kwenye Kijiji cha Vikonge ambao una wanyama wengi aina ya Sokwe kuliko wanaopatikana sehemu nyingine yoyote ile idadi kubwa kama hiyo .
Hivyo pamoja na kuwepo kwa idadi kubwa ya Sokwe wanaokadiliwa kuwa zaidi ya 3000 bado watu wengi wa nje ya nchi na ndani ya nchi hawajafahamu uwepo wa sokwe hao katika Wilaya ya Tanganyika .
Hivyo ilikuweza kuwafanya watalii wawe wanafika Wilayani Tanganyika kwa ajiri ya kuona Sokwe hao wamepanga kuanzisha utalii wa asili ambapo mambo mengi ya kiasili ya Mkoa wa Katavi yatakuwa yanaonyeshwa.
Mhando alieleza miongoni mwa mambo yatakayokuwa kuwa yanapatikana kwenye utalii huo wa asili ni mambo ya ngoma za asili za Mkoa wa Katavi .
Hivyo aliwataka wanachi wa Wilaya hiyo kujiandaa na kutumia furusa hiyo vizuri ili kuweza kujiongezea vipato vyao ambavyo vitawasaidia kuboresha maisha yao .
Afisa Maliasili wa Halmashauri hiyo Josephina Rupia alisema utalii wa Kiasili umepangwa kuwa utakuwa unafanyika katika Kijiji cha Vikonge na jamii kama jamii itanufaika na utalii huo .
Hivyo aliwataka wakazi wa Kijiji hicho kuwa tayari kuupokea mpango huo wa kuanzisha utalii wa kiasili kwa manufaa yao na kw manufaa ya watu wa Mkoa wa Katavi na Taifa kwa jumla .
0 comments:
Post a Comment