Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Taasisi ya Jane Gooddall inayojihusisha na utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa mistu imekabidhi jengo la ofisi kwa kwa ajiri ya Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Tanganyika na kwa ajiri ya Jumuia ya uhifadhi mistu na Mazingira Jumammatu A walioijenga kwa gharama ya shilingi Milioni 50.
Naibu Mkurugenzi wa wa Programu ya GMU ya Taasisi hiyo Mary Mavanza alikabidhi ofisi hiyo ya kisasa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando hapo katika afla iliyofanyika katika Kijiji cha Vikonge .
Katika taarifa yake kabla ya kukabidhi jengo hilo la ofisi Naibu Mkurugenzi huyo alisema Jumuia ya Uhifadhi mistu na mazingira Jummmatu A ni miongoni mwa jumuia sita zinazofanya kazi na Taasisi hiyo na inategemewa kwa kusimamia rasilimali za mistu .
Alisema Taasisi hiyo imewajengea jengo hilo kwa gharama ya kiasi cha shilingi milioni 50 ambapo wananchi wa Kijiji hicho wamechangia Tshs 3,195,000 lengo la kujenga jengo hilo la Ofisi ni kwa ajiri ya kufanyia kazi na kutunzia hati za viwanja za kimila zinazotolewa kijijini hapo ambapo gharamu ya upimaji ulitolewa na Taasisi hiyo .
Naibu Mkurungezi huyo alieleza ofisi hiyo itakuwa inatumiwa na Kijiji hicho pamoja na Jumuia hiyo na pamoja na kukabidhi ofisi hiyo pia walitowa pikipiki moja na mahema matatu kwa ajiri ya jumia hiyo kwa ajiri ya kufanyia shuguli zao .
Mwenyekiti wa Jumia ya Jummmatu A Abdala Kakoso alieleza kuwa jumuia hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mistu yote ilipo ndani ya vijiji vitatu wanachama inalindwa inatunzwa na kuendelezwa kwa ajiri ya matumizi endelevu ya kizazi kijacho ikiwa ni pamoja na kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji ,mistu na mazingira .
Jumuia hiyo imefanikiwa kuwa chachu ya uhifadhi na kusaidia kupunguza kasi kubwa ya uharibifu wa mistu na vyanzo vya maji katika vijiji wanachama ambavyo ni Majalila , Vikonge na Ntongwe.
Kakoso aisema kumekuwepo na changamoto ya ushirikiano mdogo kati ya jumuia na viongozi wa Serikali ya vijiji wanachama ambapo baadhi ya viongozi wa vijiji wamekuwa wakizuia doria zisifanyike .
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyia Salahe Mhando aliipongeza Taasisi ya Jane Goodall kwa michango yao na ushirikiano ambao wamekuwa wakiitowa kwa Wilaya ya Tanganyika .
Alisema Taasisi hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa kuendeleza uhifadhi wa mazingira katika Mkoa wa Katavi na kufanya uhifadhi wa mistu kuwa salama .
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo alisema mbali ya Taasisi hiyo kujenga ofisi hiyo pia imekuwa ikisaidia kutatua na kupunguza changamoto za kijamii katika Halmashauri hiyo.
0 comments:
Post a Comment