Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Mhando amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kumwandikia buarua ya kumsimamisha kazi afisa Mtendaji wa Kijiji cha Vikonge Tarafa ya Kabungu Wilaya Mpya ya Tanganyika Cristophar Maengo kwa kosa la kushindwa kukabidhi ofisi ya Kijiji kwa kipindi cha miezi mine sasa toka alivyoagizwa kukabidhi ofisi i.
Agizo hilo aiitowa hapo juzi wakati alikuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Vikonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini hapo muda mfupi baada ya kuwa amekabidhiwa ofis mpya i ya Kijiji hicho ilijengwa kwa gharama ya milioni 50 na Taasisi ya Jane Goodall ambayo pia itatumiwa na Jumuia ya Jummmata A inayojishughulisha na utunzaji wa mazingira .
Dc Mhando alisema mtendaji huyo wa Kijiji anatuhumiwa na wananchi wa Kijiji hicho kuwa ametumia vibaya michango ya wanachi wa Jijiji hicho fedha walizochanga kwa ajiri ya ujenzi wa darasa la shule ya Msingi Vikonge .
Aliwafafanulia kuwa baada ya kupata malaliko hayo yeye Mkuu wa Wilaya alifika mwaka jana kijijini hapo na kuagiza kuwa Mtendaji huyo wa Kijiji aondolewe Kijijini hapo ili kuweza kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake .
Alieleza pamoja na kutowa maagizo hayo mtendaji huyo wa Kijiji alikaidi agizo hilo na kushindwa kukabidhi ofisi kwa kipindi cha miezi mine sasa na bado ameendelea kuwepo Kijijini hapo .
Hivyo alimwagiza Mkurungezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kuhakikisha ifikapo Machi 28 mwaka huu awe amemwandikia barua ya kumsimamisha kazi mtendaji huyo nay eye Dc aewe apewe taarifa ya utelezaji wa maagizo hayo siku hiyo ya tarehe 28.
Alisisitiza kuwa sitaki tena kurudia kutoa maagizo hayo kwa mtendaji huyo anachokisubiria yeye DC ni utekeleza tuu wa agizo hilo na endapo agizo hilo la kumwandikia barua alitafanyika basi ntachukua hatua za kinidhamu kwa mtu mwenye mamlaka ambae alisitahili kuandika barua hiyo ya kumsimamisha kazi .
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hamad Mapengo alieleza kuwa ni kweli Mkuu wa Wilaya alitowa maagizo ya kusimamishwa kazi kwa mtendaji huyo wa Kijiji toka Novemba 26 mwaka jana lakini maagizo hayo yajatekelezwa hadi sasa .
0 comments:
Post a Comment