Askari wa TANAPA na wamamlaka ya Ngorongoro na TAWA wakipita mbele ya Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati wa kumaliza mafunzo ya Askari hao waliomaliza mafunzo ya mwezi mmoja katika kituo cha mafunzo cha Askari wa wanyama pori cha Mlele Mkoa wa Katavi
PICHA NA Walter Mguluchuma
Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jnerali Gaudence Milanzi amesema kuwa Hifadhi za Taifa na mapori ya akiba yanakabiliwa na changamoto nyingi za uwindaji wa wanyama wakubwa kama Tembo , Faru, kwa ajili ya pembe na vipusa pamoja na uingizwaji wa mifugo ndan i ya Hifadhi hali ambayo inathiri ustawi wa hifadhi na mapori.
Kauli hiyo ilitolewa jana wakati akifunga mafunzo ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi kwa askari 113 waandamizi wa Tanapa ,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA na TAWA yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo cha Mlele Mkoani Katavi.
Alisema kuwa kwa sasa hifadhi zetu pamoja na mapori yote yanakabiliwa na changamoto nyingi sana zikiwemo uwindaji wa wanyama wakubwa kama Tembo na Faru kwa ajili ya pembe na vipusa ,uingizwaji wa mifugo hifadhini pamoja na nyingine nyingi .
Milanzi alieleza kuwa kwa sasa Tanzania imekubwa na changamoto kubwa ya ujangili wa kutumia silaha za aina mbalimbali za moto na hasa zile za kivita hali inayoenda sambamba na matukio ya kigaidi yanayotokea maeneo mbalimbali duniani na mengine ya hivi karibuni ya unyanganyi wa kutumia silaha hapa kwetu Tanzania .
Toka taasisi za Hifadhi TANAPA na Ngorongoro zianzishwe zimekuwa kwenye mfumo wa utendaji kazi wa kiraia ambao Wizara imeona umeshindwa kutatua changamoto na matatizo mbalimbali yanayokabili uhifadhi kwa ujumla .
Alisema Wizara kwa kutambua hilo ndio maana inabadilisha mfumo wa utendaji kazi wa taasisi hizo kutoka mfumo wa kiraia na kuwa jeshi usu kwa dhamira sahihi na kwa umoja Wizara ya Maliasili na Utalii inaamini changamoto za ujangili na uingizaji wa mifugo ndani ya Hifadhi zitafikia mwisho.
Alisitiza kuwa Serikali haipendi migogoro na wafugaji na wala sio nia ya Serikali kuona watu wake wanakufa .
Aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kutokumia nguvu kubwa pale ambapo hapa sitahili hivyo watumie silaha wanazokuwa wamepewa kwa waledi na wazitumie pale inapo bidi na wananchi nao wanapaswa kutii na kufuata sheria za uhifadhi kama ambavyo zinaelekeza na waache tabia ya kuwapiga askari.
Naibu mhifadhi mkuu wa TANAPA Mtango Mtaiko alieleza kuwa mafunzo kama hayo yatakuwa yakifanyika mara kwa mara kwenye chuo hicho ili kuwafanya wasiwe wa kizamani ili kukabiliana na mbinu mpya za majangili .
Naibu Mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro Maulusu Msuha alisema mfumo mzima wa utendaji kazi unabadilika hivyo watumishi nao wabadilike na waende na wakati na watumishi wote pamoja na maafisa wao lazima wapate mafunzo ya kuwatowa kwenye mfumo wa kiraia na kuelekea jeshi usu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa mamalaka ya usimamizi wa wanyama pori aliwataka watumishi wa taasisi hizo wazingatie sheria na kanuni wanapo kuwa wakiwakamata watuhumiwa ili kuepukana na kesi na pia wafanye kazi kwa masilahi ya Taifa na wazingatie tija na usalama wa Taifa .
0 comments:
Post a Comment