Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Jumla ya Watu 88 wameungua ugonjwa wa wa kipindupindu na kati yao watu watatu wamefariki Dunia katika Tarafa ya Karema iliyoko mwambao wa ziwa Tanganyika Wilaya mpya ya Tanganyika Mkoani Katavi .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hapo jana na mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando kwa wandishi wa Habari ofisini kwake uogonjwa huo wa kipindupindu uligundulika hapo Desemba 9 ambapo mgonjwa mmoja aliungua ugonjwa huo katika kata ya Kapalamsenga ambae alikuwa ametokea katika Kijiji cha Kalya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma .
Mhando alisema mlipuko huo wa ugonjwa wa kipindupindu umetokea kwenye kata nne zilizopo katika Tarafa ya Karema mwambao mwa ziwa Tanganyia ambazo Kata hizo ni Kapalamsenga , Isengule ,Ikola na Karema .
Alifafanua kuwa toka kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo jumla ya watu 88 wameugua ugonjwa huo na watatu kati yao wamefariki Dunia na 67 wamepatiwa matibabu katika kambi maalumu zinazotowa huduma ya matibabu ya ugonjwa huo na wamerhusiwa kurudi manyumbani kwao huku watu 13 wakiwa wamelezwa wakiendelea kupatiwa mtibabu hadi sasa .
Alisema utafiti wa awali uliofanywa wa kitaalamu umebaini kuwa mlipuko huo wa ugonjwa wa kipindupindu katika Tarafa hiyo ya Karema umesababishwa na wananchi wa maeneo hayo kutokuwa na vyoo bora na watu kujisaidia haja kubwa kando kando ya ziwa Tanganyika .
Dc Mhando alitaja sababu nyingine kuwa ni wananchi wa maeneo hayo kuwa vyoo vifupi ambavyo havina mifuniko na watu kutozingatia kanuni za afya .
Alisema katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo hatua mbalimbali zimemechukuliwa kadri inavyowezekana ilikuokowa uhai wa watu kwa kuhakikisha dawa na vifaa tiba zinapatikana pamoja na rsilimali watu .
Na wameweka mkakati wa kikosi kazi ambacho kinafanya kazi ya kuhakikisha kila mtu wa Tarafa hiyo ya Karema anakuwa na choo bora na chakisasa .
Vilevele wamepenga kuwa na utaratibu wa kupulizia dawa za kuuwa wadudu kwenye vyoo vyote vya wakazi wa Tarafa hiyo na kwenye madimbwi ya maji na zoezi hilo litakuwa ni la kudumu hasa katika kipindi cha kabla ya msimu wa mvua kuanza ..
Pia wamepiga marufuku watu kutumia maji ya ziwa Tanganyika kwa kuoga na kufulia na chotoka kwa ajiri ya matumizi yao ya nyumbani na wamewaelekeza watumie maji ya bomba yalioko kwenye maeneo yao wanayoishi.
Aidha uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Tanganyika umepiga marufuku kipindi hiki cha mlipuko wa kipindupindu biashara ya pombe zote za kienyeji ,biashara za migawaha na upikaji holela wa vyakula katika misiba na sherehe mbalimbali .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment