Home » » AJALI ZA BARABARANI ZAPUNGUA MKOANI KATAVI

AJALI ZA BARABARANI ZAPUNGUA MKOANI KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter    Mguluchuma.
       Katavi


AJALI za barabarani  na ukiukwaji wa sheria za barabarani katika mkoa
wa Katavi umepungua katika kipindi cha mwaka uliopita ikilinganisahwa
na mwaka 2015 , imeelezwa .

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi , Damas Nyanda akizungumza na
waandishi wa habari katika manispaa ya Mpanda alisema kuwa kwa mujibu
wa takwimu mwaka  uliopita kulikuwa na ajali za barabanbi 65
ikilinganishwa na ajali 112 zilizotokea  mkoani humo mwak 2015.

Alisema kuwa waliokufa katika ajali za barabarani   mwaka jana
walikuwa watu  34 ikilinganishwa na watu 49 waliokufa mwaka 2015 hivyo
kufanya upungufu wa watu  15 ikiwa ni sawa na asilimia 31.

Kwa mujibu wa Nyanda watu waliojeruhiwa katika ajali za barabarani
mwaka uliopita walikuwa  85 ukilinganisha na watu 122 waliojeruhiwa
mwaka 2015 hivyo kufanya upungufu wa 37 ikiwa ni  sawa na asilimia
30.3 ya ajali za majeruhi zilizopungua.

“ Mafanikio haya yanatokana na kuendelea kuelimisha watumia vyombo vya
moto kuvikagua vyombo vyao mara kwa mara pamoja na kuzingatia sheria
za usalama barabarani kwani kauli mbiu yetu ilikuwa‘‘Hatutaki ajali,
tunataka kuishi salama’’” alisisitiza.

Kwa upande wa jail za pikipiki alisema kuwalikuwa na matukio 28  ya
ajali hizo katika mwaka uliopita  ikilinganishwa na 47 yaliyotokea
2015 ikiwa ni upungufu wa matukio 19 sawa na asilimia 40 ya kupungua
kwa ajali za pikipiki.

Akifafanua alisema kuwa watu walipoteza maisha kutokana na ajali za
pikipiki walikuwa 12 mwaka uliopita ikilinganishwa na watu 22
waliokufa kwa  mwaka juzi hivyo kufanya kupungua kwa idadi ya watu 10
waliokufa sawa na asilimia 45.45.

“ Watu waliojeruhiwa katika kipindi cha mwaka 2016 ni 26 ukilinganisha
na watu 38 waliojeruhiwa kwa kipindi cha mwaka 2015 hivyio kufanya
kupungua kwa majeruhi 12 sawa na asilimia 31.5 “aliongeza kusema ..

Alisema  ili kuhakikisha Jeshi hilo la polisi  linakabiliana na
changamoto hizo linaendelea kuelimisha watumia vyombo vya moto
kuzingatia usalama wao wawapo barabarani pamoja na kuendelea
kushirikiana wadau wengine wa usalama katika kuboresha miungombinu ya
usafirishaji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa