Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kafisha Tarafa ya Karema Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wanalazimika kusomea masomo yao huku wakiwa chini ya miti ya miembe kutokana na shule hiyo yenye mikondo saba kuwa na madarasa mawili tuu ya kusomea .
Hayo yalielezwa hapo juzi na Diwani wa Kata ya Ikola Philimoni Moro wakati alikuwa akizungumza mbele ya Wandishi wa Habari kuhusiana na changamoto zinazoikabili Kata hiyo iliyoko mwambao mwa Ziwa Tanganyika .
Alisema Shule hiyo ya Msingi Kafisha inajumla ya Wanafunzi zaidi ya 600 na inavyumba viwili tuu vya madarasa huku ikiwa na mikondo ya kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na ina Walimu saba
Kutokana na uhaba huo mkubwa wa vyumba vya madarasa wanafunzi wa shule hiyo wanalazimika kusomea chini ya miembe huku wengine wakiwa wanapigwa na jua .
Diwani Moro alisema kipindi cha mvua za masika kimekalibia kuanza hivyo yeye kama Diwani wa Kata hiyo hajui wanafunzi wa shule hiyo watakuwa wanasomea wapi wakati mvua itakapokuwa inanyesha.
Alieleza pamoja na jitihada zilizofanywa na Wananchi za kuchangia madawati katika shule hiyo ya Kafisha wananchi wanaweza wakavunjika moyo baada ya kuona madawati waliochangia yakiwa yako nje yanapingwa tuu na jua .
Nae Mbunge wa Jimbo hilo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso alikiri kuwepo kwa tatizo la upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa
Alisema tatizo hilo kwenye jimbo hilo ni la muda mrefu na ndio maana miaka mine iliyopita yeye kama Mbunge aliweza kutowa msaada wa madawati kwenye baadhi ya shule ambazo wanafunzi walikuwa wakisomea chini na pia alichangia vifaa vya ujenzi wa majengo ya madarasa .
Hivyo aliwaomba Madiwani kufanya kazi ya kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuchangia uenzi wa madarasa,nyumba za Walimu na matundu ya vyoo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment